Kadhia ya kuwakufurisha Khawariji

Egypt's Dar Al-Ifta

Kadhia ya kuwakufurisha Khawariji

Question

Je! Kadhia ya kuwakufurisha Khawariji ni ya msingi katika kuwapiga vita?

Answer

Kuwakufurisha au kutowakufurisha Khawariji hakuathiri katika hukumu ya wajibu wa kupambana na uadui wao na kuwapiga Jihadi na kupiga vita ufisadi wao, Jihadi ni faradhi katika Uislamu ili kupambana na adui yeyote, sawasawa adui huyu ni Muislamu au si Muislamu, na miongoni mwa Aya zilizo wazi katika Qur’ani  katika masuala haya ni kauli ya Mwenyezi Mungu:{Na ikiwa makundi mawili katika Waumini yanapigana, basi yapatanisheni. Na likiwa moja la hao linamdhulumu mwenzie, basi lipigeni linalo dhulumu mpaka lirejee kwenye amri ya Mwenyezi Mungu. Na likirudi basi yapatanisheni kwa uadilifu. Na hukumuni kwa haki. Hakika Mwenyezi Mungu anawapenda wanao hukumu kwa haki.}  [AL H'UJURAAT.9], Mwenyezi Mungu  Ameithibitisha Imani kwa kundi lililofanya dhuluma, pamoja na hivyo Ameamrisha lipigwe vita; kwa sababu ya kufanya uadui na dhuluma, kwa ajili hiyo tunasema: Hakika kuwapiga Jihadi Khawariji ni wajibu wa kisharia ambao ndani yake kuna thawabu kubwa kwa Mwenyezi Mungu; hilo ni kutokana na kitendo chao cha kumwaga damu za watu wasio na hatia, kufanya uharibifu ardhini na kuharibu kulikopitiliza kwa sura ya Dini Tukufu ya Uislamu,  ama suala la ukafiri na imani  hili ni – kama walivyoeleza Wanazuoni wa Fiqhi - linafungamana na mambo mengine yanayofungamana na ndoa, talaka, kumwosha maiti na kumvisha sanda, kumsalia, kumzika katika makaburi ya Waislamu, mirathi na mengineyo.

Share this:

Related Fatwas