Mapambo ya Mavazi ya Mwanamke
Question
Ni ipi hukumu ya Sharia ya Kiislamu kuhusu mavazi ya mwanamke na hukumu ya kudhihirisha nyewele zake?
Answer
Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mavazi yanayokubalika kisharia yanayotakiwa kwa mwanamke Muislamu ni yale mavazi ambayo hayaonyeshi maumbo ya mwili, hayana mwonekano wa ndani, wala hayaonyeshi sehemu za mwili. Yaani, mavazi haya lazima yaufunike mwili mzima isipokuwa uso na viganja vya mikono, na lazima yasibane wala yasioneshe maumbile ya mwili. Haikatazwi kwa mwanamke kuvaa mavazi yenye rangi, mradi tu yasivutie macho wala kuchochea fitina. Iwapo mavazi yoyote yatatimiza masharti haya, basi mwanamke Muislamu anaweza kuyavaa na kutoka nayo mbele ya wanaume wasiokuwa maharimu wake.
Hili ndilo maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu katika Suratul-Nur: { Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, } [An-Nur: 31], na pia kauli Yake katika Suratul-Ahzab: {Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wanawake waumini wateremshe juu yao jilbabu zao } [Al-Ahzab: 59]. Neno “Khimar” kwa Kiarabu linamaanisha kitu chochote anachojifunika nacho mwanamke kichwa na kifua chake. Sio lazima kiwe kile kinachojulikana na watu siku hizi kama Ushungi “khimar” kwa sura maalumu, kwani huo ni ufahamu wa kimila usiofungamana na maana ya kisharia. Kila kitu kinachositiri nywele na kifua ni khimar, hata kama hakifananani na kile kinachoitwa ushungi leo.
Kwa msingi huu, na katika hali ya swali: Inawajibika kwa mwanamke Muislamu kufunika nywele zake, kifua chake, na mwili wake wote isipokuwa uso na viganja, kwa kutumia aina yoyote ya vazi anavyopenda, na si lazima avae aina maalumu ya nguo, kwa sababu hukumu za kisharia zinahusiana na maana ya vazi, si majina yake.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
