Hukumu ya kuvaa Niqabu kwa mujibu w...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kuvaa Niqabu kwa mujibu wa Madhehebu ya Shafi

Question

Ni ipi hukumu ya kuvaa niqabu, haswa kwa mujibu wa madhehebu ya Shafii?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Nikabu si wajibu kwa mujibu wa Madhehebu ya Shafi. Na kuna kauli kuwa ni wajibu katika isiyokuwa Swala inapokuwa mbele ya watu wasio Mahrim. Hata hivyo, rai inayokubalika ni kwamba kuvaa niqabu si wajibu. Imamu Al-Mawardi amesema katika kitabu cha Al-Hawi: “Ama uchi ni aina mbili: mdogo na mkubwa. Uchi Mkubwa ni mwili mzima isipokuwa uso na vitanga vya mikono. Uchi Mdogo ni eneo kati ya kitovu na magoti.kinacholazimu kusitiri aina hizi mbili kwa ajili yake ni aina tatu: Kwanza, ni wajibu kufunika Uchi Mkubwa, hii ni  katika hali tatu: ya kwanza, wakati wa Swala, ya pili pamoja na wanaume wasio Mahrim... Tatu, pamoja na Khunthaa (Mtu mwenye jinsia mbili) asiyejulikana jinsia yake.”. Imamu Al-Nawawiy amesema katika kitabu cha “Al-Majmu’ Sharh Al-Muhadhdhab”: "Ama 'awrah ya mwanamke huru, ni mwili wake wote isipokuwa uso na vitanga vya mikono hadi kwenye viwiko viwili. Makhurasani wamesimulia kauli kwamba nyayo za miguu yake sio Uchi. Al-Mazni amesema: Nyayo za miguu ya mwanamke siyo Uchi”. Sheikh Al-Islam Zakariya Al-Ansari amesema katika kitabu cha “Asna Al-Mataleb”, kitabu cha Shafi: “Kutazama uso na vitanga vya mikono wakati hakuna ushawishi, katika kile kinachodhihirika kwa mtazamaji wa mwanamke kutoka kwa mwanamume, na kinyume chake, inajuzu, hata kama haipendezi”. Pia amesema: “Uchi wa mwanamke aliye huru katika Swala na mbele ya asiyekuwa Mahrim,” hata kama nje ya Swala, “ni mwili wake wote isipokuwa uso na vitanga vya mikono.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas