Hukumu za Aqiqah kwa mtoto wa kiume na wa kike
Question
Ni namna gani Aqiqah ya mtoto wa kiume na wa kike?
Answer
Aqiqah ni Sunna iliyohakikishwa kutoka kwa Mtume (S.A.W.) na kuwahimiza Waislamu waifuate, asili ya Aqiqah ni kuchinja mbuzi mmoja, kwa mtoto anayezaliwa akiwa wa kiume au wa kike, kwa mujibu wa alivyofanya Mtume (S.A.W.) alipozaliwa mtoto wake Ibrahim na pia walipozaliwa wajukuu wake Al-Hassan, Al-Hussein na Al-Muhsin (A.S.), kwa mujibu wa Hadithi iliyosimuliwa kutoka kwa Ibn Abbas (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.): “Alichinja kondoo mmoja kwa kila mmoja kati ya Al-Hassan na Al-Hussein kama ni Aqiqah” Imesimuliwa na Abu Dauud.
Linalopendeza zaidi ni kuchinja mbuzi wawili kwa mtoto wa kiume na mbuzi mmoja kwa mtoto wa kike, kwa mujibu wa iliyosimuliwa kutoka kwa wengi wa maswahaba (R.A.), kuhimiza kutekeleza Aqiqah kumesisitizwa katika Hadithi kadhaa za Mtume (S.A.W.), kwa hiyo akichinja mbuzi mmoja kwa kila mtoto inakubaliwa na huwa amehakikisha Sunna kwa kauli ya Ummu Kurz (R.A.) alisema: nimemsikia Mtume (S.A.W.) akisema: “Aqiqah ni mbuzi wawili kwa mtoto wa kiume na mbuzi mmoja kwa mtoto wa kike” imesimuliwa na Aswahabul-Sunan, nayo ni rai inayopendekezwa katika Fatwa.