Kuwafundisha watoto wa kike kuswali...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwafundisha watoto wa kike kuswali

Question

Je, inajuzu watoto waswali bila ya kutia udhu wala kuvaa hijabu kwa watoto wa kike wakiwa wanafundishwa Swala?

Answer

Kuwafudisha watoto kuswali wakiwa nyumbani au mashuleni kwa namna inayowafaa na kuwafanya waipende Swala na kuwajibika nayo, hata ikiwa hii kwa nia ya kuwapa mazoezi na kuwafundisha tu bila ya kujali udhu wala hijabu kwa mabinti, ni jambo ambalo wanaolisimamia wanastahili malipo mema, hasa kwa kuzingatia kuomba shauri la wadau wa saikolojia ya watoto na wale wanaohusika na kufundisha maadili na malezi bora ambao wanajitolea kuwafundisha watoto ibada mbalimbali wakiwa na subira na uvumulivu kwa lengo la kuwasaidia wale watoto kutekeleza majukumu yatakayotakiwa kufanywa nao kwa mujibu wa Sharia katika siku zao za baadaye, na hili ni sura inayofanana na subra iliyotajwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na waamrishe watu wako kusali, na uendelee mwenyewe kwa hayo. Sisi hatukuombi wewe riziki, bali Sisi ndio tunakuruzuku. Na mwisho mwema ni kwa mchamngu} [Taha: 132], na kauli yake (S.W.): {Na alikuwa akiwaamrisha watu wake Sala na Zaka, na alikuwa mbele ya Mola wake Mlezi mwenye kuridhiwa} [Maryamu: 55].

Share this:

Related Fatwas