Kuwatendea wema wazazi wawili
Question
Je! Kuwatendea wema wazazi wawili kunafuta madhambi?
Answer
Zimepokewa Hadithi tukufu nyingi kwamba madhambi hufutwa kwa baadhi ya matendo mema: kama kuwatendea wema wazazi wawili, Hija na kusimama usiku wa Laylatul Qadri… na mengineyo, miongoni mwa Hadithi hizi katika suala hili ni kauli ya Mtume S.A.W.: “Mwenye kuhiji na hakufanya uovu wala maasi atarudi kama siku aliyozaliwa na mama yake” (Hadithi hii ni Muttafaqun Alayhi). Na kutoka kwa Ibn Omar R.A. kwamba alikuja mtu mmoja kwa Mtume S.A.W. akasema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, mimi nimefanya dhambi kubwa, je! naweza kutubu? Akasema: “je! una mama?” akasema: hapana. Akasema: “Je! Una mama mdogo/mkubwa?” akasema: ndiyo. Akasema: “Basi mtendee wema” (Hadithi imepokelewa na At-Tirmidhy”.
Lakini kunatakikana kwa mwanadamu asihadaike na fadhila hizi zilizotajwa akazama katika maasi; kwa kutegemea kwamba atasemehewa kwa kuwafanyia wema wazazi wawili- na amali nyingine njema- bila ya kujuta na kuomba msamaha na toba, bali ni wajibu kwake kufanya haraka kutubu na kuomba msamaha.