Kwenda kinyume na nasafa za wazazi wawili.
Question
Ipi hukumu ya kwenda kinyume na nasaha za wazazi wawili katika kuoa?
Answer
Miongoni mwa adabu za maisha na maadili mema pamoja na uzuri wa desturi ni muoaji kutafuta ushauri wa wazazi wake kabla ya kupiga hatua katika kuoa na kuwashirikisha katika hatua zake, na kwa wazazi wawe wasaidizi kwa watoto wao wa kiume na wa kike katika kuanzisha nyumba zao maalum na huru pamoja na kubeba majukumu ya kijamii kuhusu familia mpya, mume na mke washiriki wawili katika majukumu, na wasio kuwa hao ni wasaidizi kwao pasi ya uingiliaji mbaya unaogusa familia.