Kutoa mawaidha wakati wa kuzika maiti.
Question
Je inafaa kutoa mawaidha kwa waliopo wakati wa kuzika maiti?
Answer
Hakuna ubaya kutoa mawaidha kwa ufupi yanayokumbusha kifo na maisha ya Akhera wakati wa kuzika maiti, kutoka kwa Amiri wa Waumini Ally R.A amesema: Tulikuwa kwenye mazishi eneo la Baqii, alitujia Mtume S.A.W akakaa na sisi tukakaa pembezoni mwake, kisha akasema:
“Hakuna yeyote miongoni mwenu, hakuna nafsi yeyote yenye kupumua isipokuwa imeandikiwa nafasi yake Peponi na motoni, au imeandikwa ni muovu au mwema” kuna mtu akauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, je tusitegemee kitabu chetu? Mtume S.A.W akasema: Fanyeni kwani yote ni mepesi kwa aliyeumbiwa”.