Yanayofanywa wakati wa kufikwa na kifo
Question
Ni yapi mtu anapaswa kusema wakati wa kumuona aliyefikwa na kifo?
Answer
Ni Sunna kufanya yafuatayo:
Aliyekuwepo kumtamkisha shahada mbili azitamke bila ya kumlazimisha na si kutaka kauli yake kwenye hizo Shahada, hii ndio maana ya kauli ya Mtume S.A.W:
“Watamkisheni maiti zenu neno Laa ilaaha illa Allah” imepokelewa na Imamu Muslimu.
Kumuelekeza Qibla akiwa amelalia ubavu wake wa kulia ikiwa kufanya hivyo hakutaleta usumbufu kwake, kwa matumaini kuwa yeye ni mtu wa Qibla, kwani Barraa Ibn Maarur R.A aliusiwa kuelekezwa Qibla pindi atakapo fikwa na kifo. Mtume S.A.W akasema: “Amepata jambo la kimaumbile” imepokelewa na Baihaqy pamoja na Al-Hakim.
Kumsomea sehemu ya Qu`rani Tukufu kama vile kumsomea Suratu Al-Ikhlaas na Suratu Yaasin, kwa kauli ya Mtume S.A.W:
“Wasomeeni maiti zenu Suratu Yaasin” imepokewa na Ahmad pamoja na Abu Daud.
Kumfumba macho na mdomo baada ya kuhakikisha kuwa ameshafariki ili awe katika muonekano mzuri, na kwa kauli ya Mtume S.A.W:
“Hakika roho inapotolewa hufuatwa na macho” imepokewa na Imamu Muslimu. Na hilo pindi alipoingia kwa Abi Salama R.A macho yake yakiwa wazi ndipo akamfumba.
Kumfunika ili kuzuia kuonekana na kufunika sura yake iliyobadilika kutokana na macho, Bibi Aisha R.A amesema alipofariki Mtume S.A.W:
“Alifunikwa na shuka ya mistari” na yasiyokuwa hayo miongoni mwa Sunna ambazo zimetajwa na Wanachuoni wa Umma.