Mambo yanayofanywa na kundi la Daish pamoja na wanawake
Question
Je, mambo yanayofanywa na kundi la Daish pamoja na wanawake ni kutokana na dini ya Kiislamu?
Answer
Kundi la Daish linashughulika na wanawake kwa ukatili wa hali ya juu, badala yake inajifichia sheria za Kiislamu ili kuhalalisha miamala hii isiyo ya kibinadamu. Miaka iliyopita, kundi hilo lilitoa kanuni kuhusiana na hili, likisema kwamba umri halali wa wasichana kuolewa ni miaka tisa! Na kwamba umri wa juu zaidi kwa wasichana ili wapate elimu ni miaka kumi na tano, na kundi hilo liliamuru kufanya tohara kwa wasichana na wanawake wote kuanzia umri wa miaka kumi na moja hadi arobaini na sita, bila kuzingatia maoni ya sayansi na tiba. Pia kundi hilo lilikataza kabisa upasuaji wa urembo, na kuhusu saluni za urembo, nazo ni - kama zilivyoelezwa ni - kazi ya Shetani. Na kundi hilo lilithibitisha kuwa jukumu la wanawake baada ya kuolewa ni wasionekane na hakuna haja ya wao kuhama huku na kule ili kupata vyeti na kadhalika. Na kwa ajili ya kuongeza ufadhili wa kundi, soko la watumwa lilianzishwa ambapo wanawake wanauzwa kwa jina la (sabaya)!