Ushauri kuhusu namna ya kulinda mai...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ushauri kuhusu namna ya kulinda maisha mazuri kati ya wanandoa

Question

Vipi tunaweza kulinda maisha mazuri kati ya wanandoa?

Answer

Ndoa imejengeka upole, huruma, upendo na kuzingatia hisia za wanandoa wawili yaani; mke na mume zaidi kuliko kuzingatia namna ya kuomba haki ya kila mmoja wao kutoka mwenzake, fiqhi ya kuzingatia hali halisi pamoja na tabia njema tuliyofundishwa na Mtume wetu (S.A.W.) husisitiza kuwa mke anapaswa kumcha Mungu katika haki za mumewe, na kutambua kuwa kuishi naye kwa hali nzuri na tabia njema akiwa na subira na uvumulivu wa mateso ya maisha yake ni sababu mojawapo sababu za kuingia peponi, pia mume anapaswa kutambua na kuthamini juhudi za mkewe na huduma anazozitoa muda wote kati ya kazi za nyumbani na kukidhi mahitaji ya watoto, kwa hiyo anatakiwa kuwa mpole wala asimlazimisha kufanya asiyoyaweza, kwa namna hii na kwa kuzingatia hisia hizo wanandoa wanaweza kutimiza wajibu zao na kutekeleza matakwa ya Mwenyezi Mungu na kuepukana na sababu za kugombana na kushtakiana mahakamani, bali kuishi maisha ya kawaida yenye utulivu na amani, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Yeye humpa hikima amtakaye; na aliye pewa hikima bila ya shaka amepewa kheri nyingi. Na hawakumbuki ila wenye akili} [Al-Baqarah: 269].

Hivyo, hukumu za kisheria zinazofungamana na ndoa hazichukuliwi kwa namna ambavyo kila upande kutafuta matini za kuthibitisha haki na wajibu zake au zinazomwunga mkono na kumdhihirisha katika upande wa aliye sahihi na mwenzake ni mkosa, hapo ndipo matini za kisheria huchukuliwa mbinu ya kumsumbua mmoja wa wanandoa na kumshinikiza awe mtiifu kwa matakwa na matarajio ya mwenzake bila ya kujali wajibu na haki zilizopitishwa na sheria kwa kila mmoja wao.

Share this:

Related Fatwas