Zawadi za Uchumba na Gharama za Kua...

Egypt's Dar Al-Ifta

Zawadi za Uchumba na Gharama za Kuandaa Nyumba ya Wanandoa

Question

Binti alikuwa amechumbiwa na kijana mmoja, na huyu kija akavunja uchumba, ipi hukumu ya zawadi ya Uchumba aliyoitoa? Na tulikuwa tumeshanunua samani za nyumba ya ndoa, kwa kumjulisha na kumshirikisha, sasa hivi tunalazimika kuviuza, jambo ambalo litapelekea kupungua kwa thamani yake. Je, hasara hii niibebe peke yangu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Uchumba, kukubaliwa mahari na zawadi za uchumba ni katika vitangulizi vya ndoa, na ni katika aina za ahadi, muda wa kuwa ndoa haijafungwa kwa nguzo zake na sharti zake za kisharia, na kumekuwa na desturi kwa watu kutanguliza uchumba kabla ya kufunga ndoa ili kuandaa mazingira mazuri kati ya familia mbili.

Pande moja ikivunja nia yake na ndoa ikawa haikufungwa, basi kisharia mahari inakuwa katika dhima ya mume kwa kufunga ndoa, ikiwa ndoa haikufungwa basi aliyechumbiwa hana haki ya mahari, na mchumba atarudishiwa mahari yake, ama zawadi ya uchumba alizompa mchumba wake, imekuwa ni desturi kuwa hiyo ni sehemu ya mahari; kwa sababu watu wanakubaliana kuoana, na hili linazitoa katika kuwa zawadi na zinakuwa mahari, na desturi imekuwa ikizingatiwa katika sharia ya Kiislamu, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Shikamana na kusamehe, na amrisha mema, na jitenge na majaahili}[Al-Aaraf, 199].

Na imekuja katika athari kutoka Ibn Masoud R.A.: “Wanachokiona Waislamu ni kizuri basi hicho kwa Mwenyezi Mungu ni kizuri, na wanachokiona kibaya basi kwa Mwenyezi Mungu nacho kibaya”, imetolewa na Ahmad na Al-Tayaalisy katika musnad zao.

zawadi ya uchumba ni katika mahari, na mchumba ulievunjika uchumba wake, hastahiki mahari kwa sababu si mke, mwanamke anastahiki nusu ya mahari baada ya ndoa, na akishaingiliwa anastahiki mahari yote.

Kutokana na hilo, zawadi ya uchumba inayotolewa na mchumba inakuwa ni ya mchumba akikataa mmoja wao au wote wawili kuoana, na alieyechumbiwa hastahiki kitu chochote, na hilo haliathiri kuwa kuvunja uchumba kuwa kunatoka kwa mwanamke au mwanaume.

Ama kwa upande wa samani ambazo zimenunuliwa na pande mbili, kwa maarifa ya mwanaume, basi asili ni kwamba uchumba ni ahadi tu ya ndoa, kama walivyobainisha, na ahadi hii haimfungi yeyote, na kila mmoja wao anaweza kuvunja uchumba muda autakao, hata kama hakuweka wazi sababu; uchumba ni kipindi cha maandalizi ya kuingia katika mkataba unaolazimu, na hauna athari yoyote, na maana hii haifikiwi ikiwa pande moja inatishiwa kulipa ikiwa tu uchumba kutavunjika, lakini ahadi hii ikikutana na kuvunjika kwake na vitendo vingine vilivyo nje na vinavyoasababisha madhara, basi wakati huo madhara yatalazimisha kulipa fidia, kila mmoja kwa mujibu wa kile alichosababisha, kwa kanuni isemeyo: “Usidhuru wala usijidhuru”, na kwa namna hii hukumu za mahakama zimetolewa katika mahakama za Kimisri katia kesi namba 13 ya mwaka wa 9 BC.

Na kipimo kinachowajibisha fidia ni kutaka mmoja jambo ambalo lipo nje ya desturi; kama mchumaba kumtaka aliyemchumbia kuandaa nguo za harusi, au kumtaka kununua samani maalumu ambazo hawezi kunufaika nazo kisharia  ikiwa ndoa haikufungwa, kisha akavunja uchumba, na kama hivyo pia kwa aliyechumbiwa, aliepata madhara wakati huo atathibisha kupatikana kwa madhara yaliyothibitishwa na pande nyingine kwa njia iliyowekwa na Mahakama. Na kuthibitisha kupatikana madhara na athari zake katika sura hii ni jambo linaloachiwa mahakama.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas