Hukumu ya Zawadi za Uchumba na Vyombo wakati wa (Khuluu) Mwanamke Anapojivua katika Ndoa
Question
Ni ipi Hukumu ya Zawadi za uchumba na vyombo wakati wa (Khuluu) mwanamke anapojivua katika ndoa?
Answer
Fatwa iliyotolewa na inayofanyiwa kazi na mahakama ya Misri ni kwamba mwanamke anayejivua kwa mume wake analazimika kurudisha mahari yake ambayo amepewa na mwanaume, na kusamehe haki zake za kisharia za kifedha anapojivua kwa mumewe; kwa kuchagua rai za baadhi ya wanazuoni kuhusu suala hili; na hili ili kupunguza gharama za pesa kwa mume kutokana na kutengena huku pasi na kutaka yeye mwenyewe.
Ama haki za mke za kifedha kisharia ambazo anasamehe anapoomba kujivua, ambazo zimekuja katika maelezo ya kifungu cha sheria namba 1 ya mwaka 2000 A.D. kinaleza: “Wanandoa wanaweza kuridhiana katika kujivua, wakiridhiana, na mke akafungua madai ya kuomba kujivua na akajilipia fidia na akajivua kwa mumewe kwa kusamehe haki zake zote za kifedha na kisharia, atarudisha mahari aliyopewa, na mahakama itahukumu kuwa ameachika”. Kila kilichothibiti kuwa sehemu ya mahari, kitapasa kurejeshwa kwa mume, pia gharama za kustarehe zinaondoka kwa kujivua, na matumizi ya wakati wa eda yanaondoka kwa mume; kwa sababu lengo la kuweka sheria ya kujivua ni kumhurumia mwanamke kuishi kwenye ndoa isiyo na talaka Pamoja na kutomkalifisha mwanaume mzigo wa gharama, isipokuwa haki za kifedha za kisharia ambazo zinaondoka kwa kujivua hazijumuishi haki ya malezi ya mtoto wala haki za anayelelewa.
Na sheria ya Misri imejitahidi kuchagua hukumu za kujivua katika Fiqhi ya sharia za Kiiislamu ili kufikia usawa kati ya mwanume na mwanamke; kuweka malipo kwa sababu ya kujivua, baada ya kuwa imeachiwa katika kauli za wanafiqhi, na kuihusisha katika haki za sharia ya fedha kunathibi kwa mke kwa ndoa; ili kumlinda na kutumiwa na mwanaume, na ili isibatilike kujivua, na wakati huohuo imefunga mlango wa kutumia kujivua kwa upande wa mke katika kumiliki mali za waume zao na kuwabebesha mzigo wa gharama za fedha ambazo hudaiwa, na huweza kuwa kiasi kikubwa cha pesa.
Na desturi ya kuweka orodha ya vitu vya ndani iliyozoeleka kwa watu ni hali ya kuthibitisha haki ya mke kwa mumewe, mwanamke akinunua vitu vya ndani kwa mahari yake iliyotangulizwa, iwe mume amempa mahari pesa au vitu vya ndani, vitu hivyo ni milki ya mke ikiwa ataingiliwa, ikiwa hajaingiliwa basi nusu ya vitu ndio itakuwa milki yake.
Na kawaida vitu vya ndani ambavyo anavimiliki mwanaume, vinakuwa milki yake. Imani ya dini ilipokuwa dhaifu kwa watu, na haki nyingi za wanawake kupotea, jamii ikaona haja ya kuandika orodha ya vitu vya mke, ili mwanamke anayeachika awe na dhamana ya haki yake kwa mwanaume ikiwa itazuka kutoelewana kati yao, na watu wengi wemeishi na desturi hii, na dhamana hii ikaitwa orodha, hii ni haki ya mke kwa mumewe kama deni lake kwake.
Isipokuwa kwamba ahadi hii imekuwa kwa wengi ni sehemu ya kutumia fursa pale mke anapokanusha kuwa orodha ni mahari yake pamoja na kutofautiana uahalisia na jambo ni hilohilo; orodha ya vitu vyote inaweza kuwa ndio mahari ambayo ameitoa mume kwa mke wake, na inakuwa imeandikwa katika cheti cha ndoa kuwa ni mahari inayoandikwa kiasi kidogo ili kukwepa kulipa ushuru wa thamani ya mahari iliyoandikwa katika cheti cha ndoa, na wanakuwa wameshirikaiana kwa kiwango tofauti, wakati mwingine mke ndie anaenunu orodha ya vitu vyote kwa mali yake na mali ya familia yake.
Na kwa umbanuzi huu hukumu huchukuliwa; mume akidai kuwa orodha yote au baadhi yake ni katika mahari na kuthibiti hilo, kwa maandishi au mashahidi, dalili ambazo hakimu anaziona na kuzuthibitisha atahukumu kupitia hizo, na ni wajibu kwa mke kurudisha orodha anapojivua kwa mujibu wa Fatwa inayofanyiwa kazi na mahakama; kwa kutoka kuwa deni kuwa ni malipo ya kitanda na kukubali kujisalimisha, na kwa hilo inakuwa ni mahari inayoapasa kurudishwa. Ama ikiwa haiathibiti hilo kwa hakimu basi inakuwa haki sahihi kabisa ya mwanamke; aliyejivua au asiyejivua, na haipasi kwake kumrudishia mume atakapojivua.
Ama zawadi za uchumba ikiwa desturi inazifanya kuwa ni sehemu ya mahari, basi vitarudishwa wakati wa kujivua, ama ikiwa wamekubaliana kuwa ni zawadi, basi vinachukua hukumu ya zawadi, na zawadi si mahari; hazirudishwi wakati wa kujivua.
Kutokana na hayo na swali lilivyo: kinachorudishwa wakati wa mwanamke kujivua ni kila kilichothibiti kuwa ni mahari, na kisichokuwa mahari hakirudishwi wakati wa kujivua, na kuhukumu kuwa orodha ya vitu au kitu kingine kuwa ni mahari au shemu ya mahari kithibitisho kinachofikishwa kwa hakimu kwa dalili sahihi na Ushahidi ambao utaangaliwa na kuonekana sahihi kama utapingwa; hakimu akithibitisha kuwa orodha ya vitu au baadhi yake ni mahari au sehemu katika mahari, atahukumu kurudishwa kwa mume kama ilivyotangulia kuweka wazi.
Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi
Arabic
Englsh
French
Deutsch
Urdu
Pashto
Hausa
