Hukumu ya kubadilisha nia kutoka Sw...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kubadilisha nia kutoka Swala ya faradhi kwenda Sunna au kinyume

Question

Ni ipi hukumu ya kubadilisha nia katika Swala kutoka faradhi kwenda Sunna au kinyume?

Answer

Kwa mujibu wa Sharia kupatikana kwa nia kabla ya kuanza ibada au kitendo ni jambo la msingi lililo thabiti katika Sharia, ambapo nia ni sharti la kusihi Swala kwa baadhi ya Maimamu wa Fiqhi, wakati wengine wakaifanya nguzo mojawapo ya nguzo za Swala, ama kuhusu kuibadilisha nia katika Swala, basi haijuzu kubadilisha nia ya Swala kutoka faradhi kwenda faradhi nyingine au kutoka Sunna kwenda faradhi, kwani baadhi ya Wanachuoni wa Fiqhi wanaona kuwa kubadilisha nia hubatilisha Swala nzima, wengine wakasema kuwa Swala hubadilika kuwa Sunna siyo faradhi ikiwa nia itabadilishwa, lakini kubadilisha nia kutoka  faradhi kwenda Sunna au kutoka Sunna kwenda Sunna nyingine, basi inajuzu ikiwa kwa sababu inayokubalika (udhuru) kwa makubaliano ya Wanachuoni wengine wakaona kuwa kubadilisha nia inajuzu bila ya kuwepo sababu ya kisharia.

Share this:

Related Fatwas