Kumuwakilisha mwingine katika Swala...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumuwakilisha mwingine katika Swala ya kutaka ushauri

Question

Je inafaa kuwakilisha mtu katika s

Swala ya kutaka ushauri?

Answer

Yaliyokubalika na kupitishwa kifiqhi ni kuwa Swala ya kutaka ushauri kwa Mwenyezi Mungu ni Sunna, hivyo inapendeza kwa mwenye kutaka kufanya jambo na akawa hafahamu mwisho wake wala hajui kama hilo jambo ni kheri kwake kuliacha au kulifanya, aswali Swala ya kumtaka ushauri Mwenyezi Mungu nayo ni rakaa mbili, mwenye kuswali ataleta duwa iliyopokewa kutoka kwa Mtume S.A.W ambayo ni: 

Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Maliki na Shafi wamepitisha mtu kuswali kwa niaba ya mwingine, kama vile mama kuswali kwa ajili ya binti yake na rafiki kwa rafiki yake, kutokana na kuwepo usaidizi katika kufanya jambo la kheri, kwa kauli ya Mtume S.A.W:

“Mwenye kuweza kati yenu kumsaidia ndugu yake basi na amsaidie”. Imepokewa na Muslimu.

Share this:

Related Fatwas