Kuanzisha dhana katika nyanja ya ki...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuanzisha dhana katika nyanja ya kidini.

Question

Je, kuna hatari gani ya yale yanayofanywa na harakati za Kukufurisha katika kujenga dhana potofu kuhusu Uislamu na kuzisambaza miongoni mwa watu kuwa ni sahihi?

Answer

Dhana huwakilisha matokeo bora zaidi ya mchakato wa kiakili wa kinadharia, kwa sababu dhana hizi ni zao la juhudi za kiakili zenye kuendelea na mfululizo ambao hatimaye utasababisha ujenzi thabiti na uundaji sahihi, ambao ni (dhana), na "dhana" hiyo ikawa ushahidi wa nguvu ya vuguvugu la fikra na majaribio ya kuanzisha na kujenga mifumo ya kisayansi, na hili ndilo linafanya suala la ukombozi wa dhana umuhimu wake wa kisayansi na kiakili.

Iwapo suala la ukombozi wa dhana za jumla na yaliyomo katika ujumla wake lina umuhimu wake kwa ujumla, basi limekuwa ni miongoni mwa masuala ya lazima na ya dharura kwa umma wa Kiislamu hasa kwa msukosuko usio na kifani wa viwango na dhana ambazo medani ya kielimu ya Kiislamu inashuhudia. Hatutii chumvi ikiwa tunadai kuwa hii misukosuko ni moja ya nyenzo mashuhuri zaidi za kuharibu mradi wa ustaarabu wa Kiislamu, kwa sababu inapiga fikra za Kiislamu kwa undani wake na kuunda hali ya kiakili yenye mkanganyiko mkubwa.

Tukipitia pendekezo la kinadharia la watetezi wa itikadi kali katika miongo ya hivi karibuni, tunaona kwamba siku zote wanajaribu kulazimisha mfumo mpya wa dhana ambao unajumuisha maono yake ya "Tauhidi," "Nchi za Uislamu," "Utawala," "Jihadi," na kadhalika, ili mfumo huu uweze kuwakilisha sehemu zake za kuanzia kuelekea kusimamisha mfumo wa fikra potofu ambazo ni ngeni katika sheria ya Kiislamu, na ni ngeni katika sheria zote za Mwenyezi Mungu.

Share this:

Related Fatwas