Ufananishaji Qur`ani kwa makundi ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ufananishaji Qur`ani kwa makundi ya kigaidi.

Question

Ni namna gani watu wenye msimamo mkali wanavyofanyia kazi Aya za Qur`ani Tukufu za kufanana?

Answer

Watu wa upotoshaji wanachukua suala lenye kufanana na Qur`ani ili kuwaharibia watu imani zao, na wanatumia masuala hayo ili kuwavutia wafuasi na watetezi hivyo wakatengeneza maana za Qur`ani Tukufu ili kuleta fitina na kutaka kufikia masilahi ya kidunia, na Mwenyezi Mungu Amefahamu kuwa kwenye Umma huu kutakuwa na watu wakilingania katika yanayofanana na Qur`ani Tukufu, hivyo Mwenyezi Mungu Akawakumbusha kwa kusema: {Ama wale ambao nyoyoni mwao umo upotovu wanafuata zile za mifano kwa kutafuta fitina, na kutafuta maana yake; na wala hapana ajuaye maana yake ila Mwenyezi Mungu. Na wale wenye msingi madhubuti katika elimu husema:Sisi tumeziamini, zote zimetoka kwa Mola wetu Mlezi.Lakini hawakumbuki hayo isipo kuwa wenye akili} Aal-Imran: 7, watu wa fikra za misimamo mikali wakafuata Aya wanazofananisha na wakazichukua na kuzifanya njia yao na dalili yao na mwongozo wao kwenye hukumu za dini na dunia, wakizutumia katika mitazamo yao mashirikiano yao na hali zao zote ili kuhalalisha matendo yao na kupambia uhalifu wao.

Miongoni mwa mifano ya hiyo, kikundi cha khawariji kuchukua kama ushahidi wa kubatilisha utawala kwa kutumia kauli ya Mwenyezi Mungu:{Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu} Al-Anaam: 57.

Maana inayochukuliwa katika Aya sahihi ni katika jumla yake, ama ufafanuzi unahitaji maelezo, kwa sababu hiyo Imamu Ally Ibn Abi Talib R.A aliwajibu na kuwambia: “Neno la haki linakusudiwa batili”.

Share this:

Related Fatwas