Msingi wa mfumo wa uelewa kwa makun...

Egypt's Dar Al-Ifta

Msingi wa mfumo wa uelewa kwa makundi ya kigaidi

Question

Upi msingi wa kielimu kwa watu wa makundi ya kigaidi?

Answer

Watu wa ukufurishaji wanatatizo la kukosa msingi salama na kutegemewa katika elimu na kutoa mfunzo na Fat’wa ufundishaji na ulinganiaji, nayo huitwa “Mtazamo wa piramidi iliyopinduliwa” hii inatokana na makosa katika kuanza na kumaliza, na tunagusa umbo la mitazamo hiyo katika akili za watu wa makundi ya kigaidi, ambapo mtazamo wao kwenye maandiko ya Kisharia tunakuta wanageuza ufahamu uelewa mwingi wa maisha yetu, na kulifanya jambo zuri kuwa baya, na baya zuri, na hivi ni vitendo tunaweza kuviita kwa jina la “Piramidi iliyopinduliwa” kawaida ya Piramid inalazimisha kuanza kwenye msingi unapanda kidogo kidogo mpaka unafika kwenye kilele  kama inavyofahamika katika umbile lake la kiuhandisi, mwenendo wa nadharia ya Piramid lililopinduliwa pamoja na mfumo wa kimuundo ambao umejengewa hukumu za Kisharia katika Sharia ya Kiislamu kuna makosa kwa pande nyingi ni sawa sawa kwa upande wa kimaarifa au kimfumo au kitabia za Kisharia.

Uislamu unategemea mpangilio kwa sababu mtazamo bora wa kila kitu ni ule mtazamo wa kati na Kati na wala si uliopinduliwa, ambapo wa kati na kati unatufanya tuanze la muhimu zaidi kisha muhimu, tofauti na tunachokiona katika makundi mengi ya msimamo mkali ndani ya mfumo wa elimu ya Sharia, wana tofauti kabisa na watu wa Sunna katika ulinganiaji, elimu, mafunzo na Fatwa.

Share this:

Related Fatwas