Makusudio ya Qur`ani kwa makundi ya...

Egypt's Dar Al-Ifta

Makusudio ya Qur`ani kwa makundi ya kigaidi.

Question

Hivi watu wa msimamo mkali wanazingatia maana ya Qur`ani Tukufu na makusudio yake?

Answer

Watu wa msimamo mkali Aya za Qur`ani Tukufu wanabadilisha maana yake wala hawafahamu makusudio yake, utawaona wanazichukua Aya zilizoteremshwa kwa wasio Waislamu hukumu zake wanazipeleka kwa Waislamu, na hili kwa nafasi yake linawapelekea kutoka kwenye mfumo wa Sunna za Mtume, kama vile linapelekea kugeuza mambo na uelewa na kulifanya lile ovu kuwa jema, na jema kuwa ovu, huwavisha watu na kuwaingiza kwenye fujo za kifikra, Mtume S.A.W. amesema: “Watatoka kizazi hiki watu wanaosoma Kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa ncha ya ulimi, wanatoka katika dini kwa haraka mfano wa mshale, ikiwa nitakutana nao nitawauwa kifo cha watu wa Thamudi” imepokewa na Muslim.

Na kauli yake: “Wanaisoma Qur`ani kwa ncha ya ulimi” Maana yake wanaisoma lakini hawafahamu maana yake na makusudio yake, kwa hali hiyo wanatoka kwenye jumla wa Waislamu, katika mazuri yaliyosemwa na waja wema waliotangulia kwa watu wa khawariji ni kuwa: Wametajwa katika kauli yake Mola Mtukufu: {Sema: Je, tukutajieni wenye hasara mno katika vitendo vyao? * Ni wale ambao juhudi zao katika maisha ya dunia zimepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri * Hao ni wale walio zikanusha Ishara za Mola wao Mlezi na kukutana naye. Kwa hivyo vitendo vyao vimepotea bure, na wala Siku ya Kiyama hatutawathamini kitu} Al-Kahfi: 103 – 105.

Share this:

Related Fatwas