Hukumu ya kufadhili huduma kwa malipo ya kidogo kidogo
Question
Je, inajuzu kufadhili huduma kwa malipo ya kidogo kidogo?
Answer
Kufadhili huduma kupitia benki kwa kulipa gharama zake kwa mfumo wa kidogo kidogo, kama vile katika huduma za Hija, Umrah na shughuli nyinginezo za kijamii kunaruhusiwa kisharia, sharti thamani ya hiyo huduma iwe imeainishwa hapo kabla kwa kukubaliana kwa pande mbili na kuafikiana kuhusu muda wa kulipa, ambapo huduma hizo huchukua hukumu sawa sawa na bidhaa zinazouzwa kwa malipo ya kidogo kidogo, ambapo huweza kuuzwa kwa kulipa hapo hapo au kulipa kwa mfumo wa malipo ya kidogo kidogo, kwa kutanguliza sehemu ya pesa au bila ya kutanguliza kitu, na kwa ziada (faida) katika bei ya huduma au bidhaa zinazouzwa kwa kulipwa kidogo kidogo au la.