Hukumu ya kuifadhili miradi kupitia Benki
Question
Ni ipi hukumu ya kuifadhili miradi kupitia Benki?
Answer
Kwa hakika mikataba ya uwekezaji kati ya Mabenki au taasisi au Jumuiya za Umma kwa upande mmoja na watu binafsi au taasisi kwa upande mwingine ni mikataba inayotegemea mipango na uchunguzi wa awali wa uwekezaji huo, kwa hiyo mikataba ya aina hiyo haina udanganyifu wala madhara, bali hukidhi mahitaji na maslahi ya pande zake husika, hivyo inaruhusiwa kisharia wala hakuna tatizo lolote, na haikubaliki kuitwa "Mikopo"; kwani mkopo huambatana na upole, huruma na hisani, kwa hiyo ni aina ya mikataba ya michango, ilhali mikataba ya kuifadhili mradi ni mikataba ya ufadhili na uwekezaji inayofuata mikataba ya fidia, na ikiitwa "mikopo" basi hayo yatasababisha kuchanganya na kanuni isemayo: kila mkopo unaoleta manufaa basi ni riba".