Msingi wa uhusiano kati ya Wataalam...

Egypt's Dar Al-Ifta

Msingi wa uhusiano kati ya Wataalamu na Watawala

Question

Ni upi msingi wa uhusiano kati ya Wataalamu na Watawala

Answer

Kwa hakika, msingi wa uhusiano kati ya Wataalamu na Watawala ni utiifu kwa upande wa wataalamu kwani wao ni sehemu ya raia sawa na wananchi wengine, Mwenyezi Mungu Amesema: {Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi} [An-Nisa'a: 59], pia, Wataalamu wanapaswa kutoa nasiha na shauri, Mtume (S.A.W.) amesema: "Dini ndiyo nasiha, Tukasema: kwa nani? Akasema Mtume: kwa Mwenyezi Mungu, kitabu chake, Mtume wake na kwa Maimamu wa waislamu na watu wa kawaida" [Imesimuliwa na Muslim], pia, wataalamu wanapaswa kuwajibika kwa vidhibiti na adabu ya kutoa nasiha na kushauriana na Watawala kwa mujibu wa iliyosimuliwa kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kuwa amesema: "Yeyote anaye nia ya kumshauri mwenye madaraka, basi asifanye hayo hadharani, bali anatakiwa kumshauri kisiri siri, Mtawala akikubali shauri huwa nzuri, akilikataa basi mtoa shauri huwa ametimiza wajibu wake" [Imesimuliwa na Ibn Abi Aa'sim], kwa upande wa mtawala anapaswa kukubali maoni au shauri lolote lililo sahihi, kwa kuwa yeye ndiye anayetakiwa kulipata shauri na maoni haya, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {na shauriana nao katika mambo} [Al-Imran: 159], pia imesimuliwa kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kuwa amesema: "Kwa hakika neno lililo zuri ni haki ya muumini, kwa hiyo popote lilipo basi muumini ni mwenye haki ya kulipata" [Imesimuliwa na Termidhy]

Share this:

Related Fatwas