Msingi unaojengewa uhusiano kati ya Waislamu na wasio Waislamu
Question
Ni nini msingi unaojengewa uhusiano kati ya Waislamu na wasio Waislamu?
Answer
Kwa hakika, msingi unaojengewa uhusiano kati ya Waislamu na wasio Waislamu ni amani, kuishi pamoja na kushirikiana kwa manufaa ya wanadamu wote, kwa maneno mengine; msingi huu ni: Hisani, Mwenyezi Mungu Amesema: {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} [Al-Mumtahinah: 8], uadilifu hapa katika Aya hii si uadilifu wa kawaida, kwani Muislamu anatakiwa kuwa mwadilidfu hata kwa maadui wake, Mwenyezi Mungu Amesema: {Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu} [Al-Maidah: 8], lakini maana iliyokusudiwa katika Aya ni kuwafanyia wema na kwa Hisani, wakati huo huo Mwenyezi Mungu hakuwakataza Waislamu kuwafanyia wema watu wote mpaka maadui wanaowapigana na Waislamu, bali akaifanya hisani hiyo ni Sunna pamoja na kuwakataza kuwafuata na kuwatii milele, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale waliokupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu} [Al-Maidah: 9], jambo ambalo tunaliona wazi katika Sira ya Mtume (S.A.W.) katika misimamo kadha wa kadha, kama vile; tukio la majabali makubwa mawili mjini Makkah, Suluhu ya Hudaibiya, Hadithi ya walioachiliwa huru na mengineyo.