Kutowajibika kwa kanuni za kimataif...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutowajibika kwa kanuni za kimataifa kwa madai ya kwamba zimesainiwa na wasio Waislamu

Question

Je, inajuzu kukataa kuwajibika kwa kanuni za kimataifa kwa madai ya kwamba zimesainiwa na wasio waislamu?

Answer

Haijuzu kukataa kuwajibika kwa kanuni za kimataifa kwa ya kwamba zimesainiwa na wasio Waislamu, ambapo Mwenyezi Mungu (S.A.W.) Amesema: {Na timizeni ahadi. Kwa hakika ahadi itasailiwa} [Al-Israa: 34], naye Mtume (S.A.W.) amesema: "yeyote anaye ahadi na watu, basi asiongeza wala asiondoe chochote katika ahadi hiyo mpaka muda wake imalizike …" (Imesimuliwa na Abu Daud), Pia, Mtume (S.A.W.) alikuwa na ahadi na mayahudi wa Madinah, ahadi ambayo tunaweza kuiita kwa lugha ya kisasa "mkataba wa ulinzi wa pamoja na ushirikiano wa kiuchumi" ambapo ahadi hiyo imekusanya mada kadhaa zikiwemo: "kuwa mayahudi wananufaika kwa mapato ya vita sawa sawa na Waislamu wakipigana vita mfano wa waislamu… na kwamba wafanyabiashara wa Qureish na wanaowaunga mkono hawaruhusiwi kuvuna mapato katika Madinah, na kuwa ahadi ya waislamu na mayahudi huasisiwa kuwa pamoja dhidi ya uadui wowote unaolenga  Yathrib (Madinah)", lakini mayahudi walivunja ahadi yao kama ilivyo thabiti katika historia, pia, Mtume (S.A.W.) alikuwa na ahadi na washirikina wa Makkah, ile ahadi ambayo maswahaba waliona kuwa inawapendeleza washirikina kuliko waislamu, ni ahadi ya Hudaybiya iliyovunjwa na washirikina, inajulikana kuwa mayahudi na washirikina walikuwa maadui wakuu wa waislamu katika wakati ule.

Share this:

Related Fatwas