Tofauti kati ya istilahi za mauaji ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Tofauti kati ya istilahi za mauaji na mapigano katika Uislamu

Question

Ni nini tofauti kati ya istilahi za mauaji na mapigano katika Uislamu?

Answer

Zipo tofauti kadhaa kati ya istilahi ya mauaji na mapigano katika Uislamu, ambapo tofauti ya kwanza ni kwamba neno la (Mapigano) humaanisha kushirikiana na kuwa kitendo chenyewe hufanywa na mtendaji zaidi ya mmoja, kinyume na neno la (Mauaji) ambalo halimaanishi maana hiyo. Pili; kusudio na lengo la kuruhusu mapigano ni kuzuia uadui na kuzuia dhuluma si kwa kuua, si jambo geni kutokia mauaji wakati wa mapigano, lakini mauaji si lengo kuu la mapigano kwani mapigano hisimamishwa wakati ambapo sababu zake za msingi huwa hazipo hata mapigano haya yakiwa bila muaji, jambo linaloambatana na kauli ya Mtume (S.A.W.): "Nimeagizwa kupigana na watu …." (Imekubaliwa), kwani kitenzi (Kupigana) humaanisha kuwa kitendo hufanywa kwa pamoja na watendaji zaidi ya mmoja, na neno (watu) hapa hurejelea washirikina wa Qureish na waadui wengine waliowaudhi Waislamu, na neno (nimeagizwa) humaanisha kuwa agizo hilo ni hasa kwa Mtume (S.A.W.), vile vile, kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui} [Al-Baqarah: 190], ambapo maana inayokusudiwa hapa ni kupigana na maadui mpaka uadui na madhara yao yaondolewa, na yangeondolewa madhara yao, Mwenyezi Mungu Ametuagiza katika Aya hiyo hiyo kwa kutoanza uadui.

Share this:

Related Fatwas