Tofauti kati ya Jihadi na Mapigano katika Uislamu
Question
Ni nini tofauti kati ya Jihadi na Mapigano katika Uislamu?
Answer
Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ina maana pana ambayo iko tofauti na maana ya kupigana, amabpo Jihadi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ni kufanya juhudi za kupambana na nafsi, matamanio na shetani kwa lengo la kutaka radhi za Mwenyezi Mungu ambaye Amesema: {Na wanao fanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia zetu na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema} [Al-Ankabut:69] kwa hiyo, aina kadhaa za mapigano huenda zikaitwa Jihadi katika sheria, nayo ni yale mapigano yaliyo dhidi ya maadui kwa lengo la kuzuia madhara na maudhi yao, mfano wa hiyo kupigana na wafanyao uadui kwa kusudio la kuwazuia, lakini Jihadi kwa maana hiyo hasa hukumu yake ya asili ni wajibu wa baadhi ya waislamu si kwa wote, kwa maana ya kwamba ikitekelezwa na baadhi, basi wengine hawana lawama kutoitekeleza, na huwa na masharti maalumu yaliyotajwa na wanazuoni, kinyume na Jihadi kwa maana yake pana ambayo ni wajibu kwa kila mwenye akili, pia, ipo aina ya mapigano ambayo haikubaliki kuitwa Jihadi, nayo mapigano yasiyo na masharti na sababu za kisheria, kama vile; kukosa ruhusa ya mtawala au yale mapigano yanayowalenga wasio na hatia kama wanavyofanya magaidi.