Tofauti kati ya dalili za kudhania na za yakini katika Uislamu
Question
Ni ipi Tofauti kati ya dalili za kudhania na za yakini katika Uislamu? Na kwa nini kuiweka dalili ya kudhania sehemu ya dalili ya yakini kumekuwa sababu ya itikadi kali na ugaidi?
Answer
Hukumu za kisharia za yakini ni hukumu ambazo zinasimama kama utambulisho wa Uislamu, na hazina hitilafu ndani yake, wamekubalina juu yake Waislamu wote, wa zamani na wa sasa, Mashariki na Magharibi, wakubwa wao na wadogo wao. Nazo ni kama Kaaba Tukufu ndiyo Kibla cha Swala, na Swala ya Adhuhuri ina rakaa nne, na kwamba mwanamke kufunika kichwa ni wajibu, na haya ni tofauti na hukumu za kudhania ambazo ndani yake kuna rai mbili mpaka tatu, mpaka imepokewa kutoka kwa Imamu mwenye kujitahidi katika suala moja kuna zaidi ya rai kumi na nane, tofauti hii imeakisi maisha ya Waislamu, baadhi yao wanafuata rai hii na wengine wanafuata rai ile kutokana na kusahihisha au Fatwa za Masheikh zao na zama zao. Na kosa kubwa linalopelekea itikadi kali ni kuwabana Waislamu na kuziweka dalili za kudhania sehemu ya dalili za siasa zilizokubalika na wote, na kuchagua kauli moja katika kauli hizo, kisha kupinga mwenye kufuata kauli nyingine kama kwamba si katika Uislamu! Na Wanazuoni wameeleza kwamba hakuna kupinga katika jambo lenye tofauti ndani yake.