Msingi wa mahusiano ya kibinadamu

Egypt's Dar Al-Ifta

Msingi wa mahusiano ya kibinadamu

Question

Je, Msingi wa mahusiano ya kibinadamu katika Uislamu ni amani ama vita kama wanavyodai magaidi?

Answer

Kwa hakika, msingi wa mahusiano ya kibinadamu katika Uislamu ni amani si vita kama wanavyodai makundi ya kigaidi, Mwenyezi Mungu Amesema: {Basi wakijitenga nanyi, wasipigane nanyi, na wakakuleteeni amani, basi Mwenyezi Mungu hakukupeni njia kupigana nao} [An-Nisaa: 90], hayo yanathibitisha kuwa mapigano katika Uislamu hayaruhusiwi ila kwa sababu ya kuzuia uadui tu, na katika hali ya kuwa maadui kutowashambulia Waislamu, basi Waislamu hawaruhusiwi kupigana nao, Mtume (S.A.W.) amesema: Muislamu wa kweli ni yule ambaye watu hawapati adha kutokana na ulimi wake na mkono wake, na muumini ni yule ambaye watu wamesalimika kutokana na damu na mali zao" [Imesimuliwa na An-Nasaiy], Mwenyezi Mungu Amechagua jina la Uislamu kwa dini yake, na uadui wa pekee unaoendelea katika Uislamu ni uadui uliopo kati ya Muislamu na nafsi yake inayomshawishi kwa kufanya maovu, kisha uadui wake na shetani, kutanguliza nafsi kabla shetani kwa kuwa nafsi iko karibu zaidi kwa mtu katika hali zake zote na kuwa inamwathiri sana, pamoja na hayo nafsi inaweza kuwa sababu ya kufanya mema kupitia kuizoesha katika mema, lakini shetani hutoweka na kutupwa mbali kwa kujikinga naye.

Share this:

Related Fatwas