Misingi ya kuunganisha Undugu

Egypt's Dar Al-Ifta

Misingi ya kuunganisha Undugu

Question

Ni ipi misingi ya kuunganisha Undugu

Answer

Mwenyezi Mungu ameamrisha kuunganisha undugu, na ameamrisha hilo katika Aya nyingi za Qur'ani Tukufu, na kwa upande wa Kisharia jambo la kuunganisha undugu linatafautiana katika namna yake kwa kutafautiana wakati na mazingira, mtu na mtu mwingine, hivyo inakuwa sawa na inavyofahamika na watu vile inavyokuwa wepesi kuunganisha, kama vile kutembelea au aina yeyote ile ya kuunganisha kwa njia ya mawasiliano ya sasa.

Kauli sahihi ni kuwa ndugu ni wale watu wa karibu kwa upande wa wazazi wawili, hivyo mwanadamu anapaswa kuunganisha ndugu yake na kumtendea haki hata kama amekata undugu naye ili aweze kupata malipo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.

Share this:

Related Fatwas