Historia ya ukufurishaji katika umm...

Egypt's Dar Al-Ifta

Historia ya ukufurishaji katika umma wa kiislamu

Question

Kwa sababu gani ukufurishaji umeenea na kutajwa sana na makundi ya kigaidi kiwazi?

Answer

Kuwahukumu Waislamu ukafiri ni jambo ambalo limeanza kujitokeza tangu zama za Al-Khawariji, ambao wako mbali na mafunzo ya dini na uongofu wa Mtume (S.A.W.) japokuwa wanaamini na kukiri kuwa yeye ndiye Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumfuata ni nguzo ya pili ya dini na sehemu ya pili ya Shahada, mwanzo wa tabia ya kuwahukumu waumini ukafiri ulikuwa kwa mtu aitwaye Dhul-Khuwaisirah Al-Tamimiy, ambapo Bukhary na Muslim wamesimulia hali ya kwamba matini ni ya Muslim, kuwa Abu Saidi Al-Khodriy amesema: "Tulikuwa tumekaa na Mtume (S.A.W.) akiwa anatugawia mali fulani, akaja mtu anayeitwa Dhul-Khuwaisirah, naye ni mtu wa kabila la Banu Tamim akasema: Ewe Mtume, hakikisha uadilifu! Akasema Mtume: Ole wako!, ni nani atakayegawa kwa uadilifu kama si mimi, hakika nisingekuwa mwadilifu ningepata hasara kubwa, naye Omar bin Al-Khattaba akasema: Ewe Mtume! Niruhusu kumuua! Akasema Mtume: umwache, kwa kweli ana marafiki ambao wanasimamisha Swala vizuri zaidi kuliko nyinyi, na kufunga saumu vizuri zaidi kuliko nyinyi, wanasoma Qur`ani bila ya kutekeleza mafunzo yaliyomo ndani yake, wanatoka katika dini kama unavyotoka mshale katika upinde, …wanajitokeza wakati ambapo watu wako katika mfarakano na hitilafu kubwa", Abu Saidi akasema: "Kwa hakika nakiri kuwa nimesikia haya kutoka kwa Mtume (S.A.W.) na nakiri kuwa Ali bin Abi Twalib (R.A.) alipigana nao na mimi nilikuwa mmoja wa jeshi lake".

Katika siku za hivi karibuni, fikra za makundi haya zimekuwa na kufikia kiwango cha juu cha upotofu kupitia vizazi vinavyofuatana na hufikia  kizazi kimoja kuwahukumu kizazi kingine ukafiri, jambo linaloitwa "Nadharia ya vizazi vinavyofuatana", lakini sababu kuu ya hayo ni kukosa rejeleo sahihi linaloweza kuwaelekeza watu kwenye fikra sahihi, hivyo fikra potofu zikaenea sana kuanzia Ikhwaan, kisha wafuasi wa mkondo wa Salafi wenye msimamo mkali mpaka Daesh na wengine.

Share this:

Related Fatwas