Kugawanyika ulimwengu katika Fiqhi ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kugawanyika ulimwengu katika Fiqhi ya Kiislamu

Question

Upi msimamo wa Wanachuoni kuhusu kuzigawa nchi za ulimwengu sehemu nyingi?

Answer

Jamhuri ya Wanachuoni wamegawa nchi duniani kati ya nchi ya Kiislamu nchi ya vita na nchi ya makubaliano utulivu na upatanishi, watu wa Imamu Abu Hanifa wanaona kuwa nchi duniani zimegawanyika kwenye nchi za “Uislamu” na nchi za “vita”, na kuna kundi lingine la Wanachuoni wamegawa nchi za dunia kati ya: Nchi ya “Amani” nchi ya “Vita” nchi ya “Upatanishi” nchi ya “Makubaliano” na nchi ya “Usalama”, na wakasema kuwa: Kwa vile nchi – kwa maana nchi yeyote – kunasimamishwa ibada ya Swala katika hali ya kawaida ndani ya nchi hiyo hata kama itakuwa si nchi ya Waislamu basi katika hali hii itazingatiwa ni nchi ya amani na usalama, na wala si nchi ya vita, kama vile wameeleza pia kuwa nchi yeyote iliyomo kwenye sheria za Umoja wa Mataifa hiyo ni nchi ya “Makubaliano” na wala si nchi ya vita, na nchi nyingi duniani katika zama hizi kwa ukweli ni nchi za usuluhishi na utulivu, na hilo ni kwa kuishi ndani yake Umma wa Kiislamu pamoja na wengine si Waislamu kwa makubaliano na mikataba ya Kimataifa, na kutokana na hali hiyo huzingatiwa ni nchi ya amani na wala si nchi ya Uislamu, kwa sababu nchi ya Uislamu ni ile ambayo inaongozwa na Waislamu.

Share this:

Related Fatwas