Kusafiri kwenda nchi si ya Kiislamu...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusafiri kwenda nchi si ya Kiislamu

Question

Ipi hukumu ya kusafiri kwenda nchi isiyo ya Kiislamu na kuishi huko.

Answer

Kusafiri kwenda nchi ambayo wakazi wake wengi si Waislamu Kisharia hakuna kizuizi, madamu sababu ya hiyo safari ni kufanya mambo halali, kama vile kusafiri kwa lengo la kusoma au kufanya kazi au kufanya biashara au kutembea na mfano wa hayo, pamoja na Muislamu anapaswa kuchunga usalama wa dini yake ili asijefitinishwa nao au kufitinishwa yeye mwenyewe pamoja na heshima yake, ahakikishe usalama wa kutolazimishwa kuacha dini yake au kufanya mambo yaliyoharamu Kisharia kama vile kunywa pombe au kufanya mambo machafu kama vile uzinifu au wizi na mengineyo miongoni mwa yale yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kuendeleza mambo ya dini yake kwa uhuru na amani bila ya kizuizi, nao ni wajibu wa Kisharia ambao hauna tofauti ndani yake kama vile kudumisha ibada za Swala za lazima, ikiwa yatafikiwa haya yote basi Waislamu kuishi ndani ya nchi si ya Kiislamu inafaa, dalili ya hilo ni pamoja na Mtume S.A.W. alimruhusu baba yake mdogo Abbas Ibn Abdul-Mutwalib kuishi Makka kabla ya kufunguliwa kwake, hilo ni kwa sababu ya usalama wake na kutokuwa na hali ya wasiwasi wa fitina katika dini yake.

Ikiwa masharti haya yatakosekana kwa msafiri basi ni haramu kwake kusafiri.

Share this:

Related Fatwas