Kuzuiliwa damu ya Waislamu
Question
Je kwa kufanya tu maasi au kuwa na imani dhaifu kuna halalisha damu ya Muislamu ambayo ameshuhudia kuwa hakuna mola wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wetu Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu? Na je kwa shahada hiyo tu inakubalika kwa Mwenyezi Mungu au hapana?
Answer
Wanachuoni wa huko nyuma na waliofuata baada yao wamekubaliana moja kwa moja wasifu wa Uislamu kwa kila mwenye kutamka Shahada mbili, hivyo basi damu yake mali yake na heshima yake vimezuiliwa kudhuriwa hata kama atakuwa ni mtu mwasi, kwani Mtume S.A.W. ameelezea katika Hadithi iliyopokewa na Abu Daudi kutoka Anas Ibn Malik hali ya maasi na dhambi ni katika masuala ya imani. Mtume S.A.W. amesema: “Mambo matatu ni katika asili ya Imani: Kujizuia kwa mwenye kutamka: Hakuna mola wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, wala tusimkufurishe kwa dhambi, wala tusimtoe kwenye Uislamu kwa matendo” Imepokewa na Abu Daud.
Pamoja na kusisitiza juu ya umuhimu wa kufanya matendo mema na uzito wake, na kutopuuza na kudharau katika kufanya maasi.
Kilicho haki ni kuzui mikono kushambulia watu waliotamka Shahada mbili bila ya kuwataka tofauti na hivyo ili kuziokoa nafsi zao na kukiukwa utukufu wao na kumwagika damu zao, kwani Mtume S.A.W. hakuweka sharti la kuingia katika Uislamu isipokuwa kutamka Shahada mbili tu, na alikuwa anasema:
“Mwenye kuswali Swala yetu, akaelekea Qibla yetu, akala chinjo letu basi huyo ni Muislamu ambaye ana usimamizi wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, hivyo msimkiuke Mwenyezi Mungu katika usimamizi wake”.