Kuzuia masilahi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuzuia masilahi

Question

Je, nini hukumu ya baadhi ya wafanyakazi kuzuia maslahi ya watu pasipo na haki?

Answer

Mfanyakazi wa serikali ni mfanyakazi anayelipwa ndiye anayekabidhiwa kazi aliyopewa. Kutoitekeleza kazi yake hii kwa namna inavyotakiwa wakati akichukua mshahara kwa ajili ya kuifanyia kazi ni usaliti wa amana ambayo alikabidhiwa. Mtume (S.A.W) amesema: “Alama za mnafiki ni tatu: anapozungumza husema uongo, anapotoa ahadi hukhalifu (hatimizi), na anapoaminiwa hufanya khiyana” (Imepokelewa kutoka kwa Imamu Al-Bukhari).

  Pia, kuzuia maslahi na kazi, au kuichelewesha, au kutozitekeleza kwa njia inayotakiwa ni kula pesa isivyo haki. Haya tumeharamishwa hivyo kwa kauli yake Mwenyezi Mungu: “Enyi mlio amini! Msiliane mali yenu kwa dhulma, isipo kuwa iwe biashara kwa kuridhiana wenyewe.” [An-Nisaa: 29].

Haijuzu kuzuia kazi baadhi ya wafanyakazi kwa manufaa ya wananchi bila haki. Mwenye kufanya hivyo ni lazima atubu kwa Mwenyezi Mungu, ili mapato yake yawe halali.

Share this:

Related Fatwas