Kuhudhuria Mazishi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuhudhuria Mazishi

Question

Ni ipi hukumu ya kuhudhuria mazishi na ni yapi ya kupendeza na adabu za jumla kwa hilo?

Answer

Sharia Tukufu imehimiza kuhudhuria mazishi, nayo ni moja ya Sunna zinazohitajika kwa mujibu wa Wanachuoni wengi, na kwenda kuzika ni haki ya Muislamu juu ya nduguye. Hili linahitaji mambo kadhaa, ikiwa ni pamoja na:

1. Kumswalia marehemu, kubeba jeneza lake na kufuata msafara wake wa mazishi, kuufuata mpaka kuzikwa.

2. Kumbeba marehemu hadi kaburini kwa haraka.

3. Kuwa na unyenyekevu.

4. Pasiwepo na kilio wala kelele.

  5. Kutozungumza kuhusu mazungumzo ya kidunia wakati wa mazishi yake.

6. Inapendekezwa kusimama kwenye kaburi la marehemu, kuomba msamaha na kumwombea kwa rehema na uthabiti.

Mwenye kutimiza haya yote atapata malipo makubwa na thawabu.

Share this:

Related Fatwas