Kuosha Maiti

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuosha Maiti

Question

Ipi hukumu ya Kisharia katika kushiriki asiyehitajika kwenye kuosha maiti?

Answer

Inapendeza kuhusisha muoshaji maiti na msaidizi wake tu, na inachukiza kushiriki asiyehitajika katika uoshaji.

Inapendeza yule ambaye anahudhuria kuosha maiti ni yule tu muoshaji na msaidizi wake katika kuosha, na inachukiza kushiriki asiyehitajika kuhudhuria, kwani mwanadamu kwa asili ya hali yake hapendi kuangaliwa tupu yake na yeyote, siku zote anachopenda ni kulinda utukufu wake, ni sawa sawa akiwa hai au amekufa, Sharia ya Kiislamu imekuwa na shime kubwa ya kulinda utukufu wa maiti na kuhimiza hilo, Mtume S.A.W amesema:

“Mwenye kuosha maiti akatekeleza uaminifu, wala hakueneza yaliyokuwepo kwa maiti wakati wa kumuosha, basi anaondoshewa dhambi zake na kuwa kama siku aliyozaliwa na mama yake” Imepokewa na Imamu Ahmad.

Share this:

Related Fatwas