Kutozaa watoto

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutozaa watoto

Question

Je, ni ipi hukumu ya kukubaliana kwa wanandoa kutozaa watoto kabisa?

Answer

Kutozaa watoto ni haki kwa wanandoa wote wawili, na inajuzu kwao kuafikiana ikiwa ni kwa maslahi yao binafsi, wala haijuzu kwa yeyote katika wao kufanya hivyo bila ya ridhaa ya mwenzake. Hii inaruhusiwa kwa kiwango cha mtu binafsi, kwa sababu zifuatazo:

- Kwa sababu hakuna matini katika Kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu Qur`ani inayokataza kuzuia au kupunguza uzazi.

- Makubaliano yao ya kutozaa watoto katika hali hii hupimwa kwa kutengwa / kutolewa nje mbegu za uzazi. Wanachuoni walio wengi wameafikiana kuwa kutengwa / kutolewa nje mbegu za uzazi kunaruhusiwa iwapo wanandoa wanakubali hilo.

Katika kiwango cha kitaifa, hairuhusiwi kutozaa watoto kabisa. Kwa sababu inavuruga usawa ambao Mwenyezi Mungu alianzisha uumbaji, na hii haijumuishi hatua zinazochukuliwa na nchi kushughulikia udhibiti wa uzazi, kwa yafuatayo:

- Katika kutafuta maisha bora kwa watu wake, kulingana na tafiti zinazoonesha uwezo wa nchi hizi.

- Pia, tabia ya mlezi inategemea maslahi yake.

Share this:

Related Fatwas