Kutukuza watu.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutukuza watu.

Question

Namna gani tunafahamu katika vikundi vingi vya ukufirishaji na ugaidi msingi wa “Usikivu na Utiifu”?

Answer

Usikivu na utiifu au kutukuza watu ni katika matatizo hatari zaidi ambayo yanazingatiwa mtanziko wa kifikra kwa baadhi ya vijana wanaotafuta ufuasi wa dini na kuwajibika Kisharia, na hasa pale inapokuwa vyanzo vya kupokea kwao ni kutoka kwa baadhi ya watu wa itikadi, kwani hao watu wanaamini kuwa wao wanazungumza lugha ya Sharia, na wanakwenda mbali zaidi kuunganisha kati ya Sharia na huyo mtu na kuunganisha mtoa mafundisho na huyo mtu mpokea mafundisho, badala maneno yake kuelezea mtazamo wake au ufahamu wake wa Sharia yanakuwa ndio Sharia yenyewe, kisha mpokeaji hutakasa maneno yake bila ya kuhisi, haya hurahisisha kukubali fikra zinazolinganiwa na wawakilishi wa vikundi vya misimamo mikali bila ya kufikiri, na huzingatiwa hilo ni katika ushiriki wa kifkra kati ya mifumo ya vikundi vya misimamo mikali.

Kundi la udugu wa Waislamu limezidi zaidi ya vikundi vingine katika kuongeza na kuimarisha msingi huo wa “Usikivu na Utiifu” kama moja ya misingi ya mfumo, na ambayo haimpi nafasi mfuasi wa kundi zaidi ya kushikamana nao kikamilifu, jambo linalohamisha huo utakasifu upande wa mfumo pembezoni mwa upande wa kifikra.

Kwa sababu hiyo Fatwa kutoka kwa hawa watu inakuwa ni moja ya vifaa muhimu ambavyo hutumiwa na vikundi vya misimamo mikali katika kufikia malengo yake, kila zinapoongezeka hizo Fatwa husaidia upande wa msimamo mkali, na hasa Fatwa ambazo zinachochea ubaguzi na kuchukia wengine.

Share this:

Related Fatwas