Kutekeleza nadhiri

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutekeleza nadhiri

Question

Ni ipi hukumu ya nadhiri ikiwa aliyeweka nadhiri hakuweza kutekeleza nadhiri yake?

Answer

Mwanadamu akiweka nadhiri na hakuweza kuitekeleza, au aliweka nadhiri na hakuianisha ni nini; katika hali hii ni wajibu kwake kafara ya yamini; kwa kauli ya Mtume S.W.A: “Mwenye kuweka nadhiri na hakuitaja basi kafara yake ni kafara ya yamini, na mwenye kuweka nadhiri katika kumuasi Mwenyezi Mungu basi kafara yake ni kafara ya yamini, na mwenye kuweka nadhiri na hakuiweza, basi kafara yake ni kafara ya yamini, na mwenye kuweka nadhiri na anaiweza, basi aitekeleze”, nako ni kama ifutavyo:

Kwanza: kulisha masikini kumi au kuwavisha; na hilo katika mipaka ya uwezo wake; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu katika kuelezea kafara ya yamini: “Basi kafara yake ni kuwalisha masikini kumi kwa chakula cha wastani mnacho walisha ahali zenu, au kuwavisha, au kumkomboa mtumwa. Asiye pata hayo, basi afunge siku tatu” na kunajuzu pia kutoa thamani ya chakula au mavazi kwa masikini wenye kuhitaji.

Pili: Mwenye kushindwa kutoa kafara katika njia ya chakula au mavazi kwa masikini au thamani yake; basi niwajibu kwake kufunga siku tatu.

Share this:

Related Fatwas