Kutekeleza kanuni na sheria za kazi
Question
Je ni lazima kutekeleza kanuni na sheria za kazi?
Answer
Katika mambo yanayojenga mahusiano kati ya mfanya kazi na muajiri ni makubaliano yaliyopo kati yao, hivyo ni lazima kila mmoja kutekeleza yaliyomo kwenye vipengele vya makubaliano pamoja na kutekeleza masharti, kuongezea pia umuhimu wa kuangalia kanuni na sheria za kazi zenye kulinda masilahi ya pande zote, hii ni kutokana na uwepo wa amri ya kutekeleza mikataba na makubaliano.