Kuwekeza Mali za Zaka

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuwekeza Mali za Zaka

Question

Kuwekeza Mali za Zaka

Answer

Imeandikwa Na:

Hisham Rabii Ibrahimu

Mtafiti idara ya tafiti za Kisharia

Yaliyomo kwenye Maudhui

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, rehma na amani zimuendee Mtume wetu Muhammad mfunguzi wa yaliyofungwa, mtetezi wa haki kwa haki, muongozo kuelekea njia ya Mwenyezi Mungu iliyonyoka, rehma na amani za Mwenyezi Mungu ziwe kwake na kwa watu wa nyumbani kwake na Maswahaba wake wote.

Baada ya Utangulizi:

Mali ni uti wa mgongo wa maisha, Sharia imefanya ni katika vitu muhimu ambavyo kukosekana kwake huharibu maisha ya mwanadamu na kuwa masikini, hivyo Sharia haijajisahau kuratibu umuhimu huu na kumsaidia mwanadamu kutekeleza nafasi yake katika maisha kama vile alivyotaka Mola wake, Sharia ikaamrisha miongozo mbalimbali kwa vitendo ikiwa ni kulinda umuhimu wa mali kutoharibika, na kubakia uwiano kati ya watu masikini na matajiri.

Miongoni mwa Sharia muhimu ambazo zimewekwa na Uislamu: Ni Sharia za Zaka, nayo ni mfumo wa usimamizi unaofanya kazi ya kulinda mali kama kitu muhimu kupitia uzalishaji wake – kwa maana ya Zaka – kwa kuleta uwiano kati ya masikini na tajiri, hivyo Zaka imekuwa nguzo katika nguzo za Uislamu.

Katika utafiti huu unazungumzia masuala yanayojitokeza ya Zaka na kadhia zake ambazo ni: “Uwekezaji mali za Zaka” masuala haya yametafitiwa katika wigo wa mjumuiko wa Wanachuoni na Watafiti wa mambo ya Fiqhi ya Kiislamu, kulifanyika makongamano jumuishi na makongamano ya Kifiqhi ili kuangalia hukumu ya kadhia hii, hasa katika vituo na mamlaka maalumu za ukusanyaji wa Zaka.

Katika utafiti huu nimejaribu kukusanya yaliyosemwa katika masuala haya na utafiti wake wa Fiqhi linganishi, lengo langu katika utafiti huu halikuwa kuleta ufumbuzi wa kina wa kiuchumi kuhusu namna ya uwezekazaji mali za Zaka, kwani hilo linaelezewa na watu wake, na kumpa msomaji nafasi kuangalia moja ya tafiti ambazo zimeandaliwa na mmoja wa Wanauchumi naye ni Dr. Faris Masduud Mkuu wa Kitivo cha Sayansi ya Uchumi Chuo Kikuu cha Blida nchini Algeria, kwa jina la “Mkakati wa uwekezaji mali za Zaka” katika utafiti huu umezungumzia baadhi ya miundo ya ufadhili ambayo inawezekana kukidhi matashi ya mwenye kutaka kuwekeza mali za Zaka.

Maelezo ya utafiti huu kwa umuhimu wake yamegawanyika sehemu mbili zifuatazo:

Sehemu ya Kwanza: Maana ya Uwekezaji.

Sehemu ya Pili: Hukumu ya uwekezaji mali za Zaka, pia inakusanya masuala yafuatayo:  

Masuala ya Kwaza: Uwekezaji mali za Zaka kwa wanaostahiki.

Masula ya Pili: Uwekezaji mali za Zaka kwa mmiliki wa kwanza.

Masuala ya Tatu: Kuwekeza mali za Zaka kwa kiongozi au anayekaimu nafasi yake.

Kisha sehemu hizi mbili zikafuatiwa na maamuzi ya majopo ya Wanafiqhi na mamlaka za Kisharia kuhusu masuala ya tafiti.

Namuomba Mwenyezi Mungu Mtukufu awezeshe na aniepusha na makosa. Amin

Sehemu ya Kwanza

Maana ya Uwekezaji.

Neno uwekezaji katika lugha ya Kiarabu lina maana nyingi zinakusanywa na: Uwingi au Mapato, uwekezaji maana yake ni kutaka mazao, asili hii ina maana nyingi, miongoni mwake ni: Mazao ya mti, uwingi wa mali, kwa mfano unaweza sema mtu amezalisha mali yake, kwa maana ameisimamia vizuri na kuikuza, miongoni mwa maana zake pia ni: Mtoto, kwa sababu mtoto ni zao la baba yake, kwa maana amezaliwa na yeye, maana nyingine: Aina za mali. Mwenyezi Mungu Amesema:

{Naye alikuwa na mazao mengi. Basi akamwambia mwenzake naye akibishana naye: Mimi nimekushinda wewe kwa mali na nguvu za watu} [AL KAHF 34]

Kwa maana ya mali nyingi zenye faida, na husemwa kila manufaa yatokanayo na kitu ni: Mazao yake, kama kusema: Zao la elimu matendo mema, zao la matendo mema Pepo ([1]).

Maana ya uwezekezaji kilugha imepokewa katika vitabu vya Wanafiqhi, lakini ni mara chache sana kuelezewa kwa tamko la “Uwekezaji” bali wameelezea kwa matamko mengine, miongoni mwa matamko hayo ni “Uzalishaji” na “Kukuza” kwa maneneo hayo wamekusudia kile kinachoongeza mali.

Imamu wa Misikiti Miwili anasema: “Kilimo cha umwagiliaji hufanana na mkopo katika makusudio, hufungamana na kisichokuwepo, na uwezekano wa kutofahamika katika mapato, ufafanuzi wa hilo ni kuwa: Makusudio ya mkopo ni uwezekano wa mkopaji kupata faida, ambapo wakati mwingine wakopaji wanashindwa kufanya vizuri kwenye mikopo yao kisha mkopo unakuwa na riba inayosubiriwa, vile vile makusudio ya kilimo cha umwagiliaji ni mwenye ujuzi kufanya kazi za mimea na miti, ambapo watu wengi wanakosa ujuzi wa namna ya kulima mimea na miti kiuwekezaji” ([2]).

Na Imamu Fakhru Zailai anasema: “Kiongozi ameamrishwa kukuza hazina ya nchi kwa njia yeyote inayomuwezesha” ([3]).

Na Badrul-Ainii anasema katika kusherehesha kauli ya mwenye kitabu cha Al-Hidaya:  “Lau mmea utaota na hakupata mazao, basi ardhi haitakuwa na deni mpaka avune mazao”, ameeleza hayo kwa ufupi bila kutaja ndani ya kitabu ikiwa mkulima amelima kisha mimea haikuota na akakutana na deni kubwa la mwenye shamba ipi hukumu yake. Katika kitabu cha Dhakhira Masheikh wametofautiana. Sheikh Abubakri Al-Itaabi amesema: Kwake itakuwa hivyo, kwa sababu huyu mweye kulima hana pesa itokanayo na kilimo, kwa sababu kulima ni matumizi, na kwa sababu hii wamesema, mwenye kulima anaweza kuvunja mkataba wa kilimo. Na Sheikh Abu Is’haqa Al-Hafidh amesema: Hapaswi kufanya hivyo, kwa sababu kilimo ni uwekezaji na wala si matumizi ([4]).

Na Sheikh Zakaria Al-Ansar anasema kuhusu masharti ya kilimo cha umwagiliaji: “Haifai isipokuwa kwa mazao maalumu ya kumwagilia kama kilimo cha tende na zabibu, kwa sababu zao la tende ndani yake kuna zaka na kukadiriwa matunda yake, hivyo inafaa umwagiliaji katika mazao haya mawili, ikiwa ni juhudi katika kuzalisha mazao hayo mawili kwa masilahi ya mmiliki mtumiaji na watu masikini” ([5]).

Na Imamu Kasany anasema: Kauli yake “Mwenye kumsimamia yatima basi atoe Zaka ya mali yake” kwa maana: Atumie katika mali ya yatima ili ipate kukuwa, kwani kutoa Zaka ni kukuza mali” ([6]).

Ama uwekezaji katika mazoea ya kiuchumi kumekuwa na fasiri nyingi zenye kukubaliana, miongoni mwa fasiri hizo ni pamoja na iliyoelezewa na mwenye kamusi ya kiuchumi kuwa: “Kuhusisha mtaji ili kupata njia mpya za uzalishaji, au kuboresha njia zilizopo kwa lengo la kuongeza nguvu ya uzalishaji” ([7]).

Ama kamusi elezi ya uchumi fasiri yake ni kuwa: “Matumizi yanayofanywa na mwenye kazi ili kulinda au kuboresha uzalishaji wake ambao unaelezea kuhamisha mtaji wa fedha na kuwa mtaji wenye kuzalisha, na katika mradi hufahamika uwekezaji ni kuhamisha pesa na kuzipeleka kwenye kazi kama vile viwandani au kwenye mashine mbalimbali nk kwa lengo la kuongeza uzalishaji na kupata faida kubwa” ([8]).

Na ikaelezewa na kamusi ya misamiati ya kiuchumi kuwa: “Kutengeneza mtaji mpya ambao unakuwa ni ongezeko la nguvu ya uzalishaji, nayo ni ongezeko safi katika mtaji kwa jamii, na vipengele vyake ni pamoja na majengo ujenzi vifaa mitambo usafirishaji wanyama na ardhi” ([9]) ([10]).

Na Jopo la Wasomi wa lugha ya Kiarabu wameelezea Ni: “Kutumia mali katika uzalishaji ima wa moja kwa moja kwa kununua vifaa, au kwa njia isiyo ya moja kwa moja kama vile kununua hisa na bondi” ([11]).

Fasiri zote hizi zinakaribiana, na zinaeleza maana ya uwingi na ukuzaji – nayo ndio maana ya kilugha ya uwekezaji – tofauti na fasiri mbili za mwanzo – nazo ni fasiri ya kamusi ya kiuchumi na kamuzi elezo ya uchumi – zimeongeza maana ya ziada ya fasiri mbili zingine, nayo ni kulinda mtaji uliopo kwa kuweka vifaa ambavyo vitasimamia kubakia kwa mtaji bila kupungua nayo ni aina ya uwekezaji, hata kama haijaeleza maana ya kuongezeka au uwingi.

Kwa maelezo yaliyopita, kusudio la uwekezaji wa Zaka ni:  “Kuongeza na kukuza mali ya Zaka kupitia vifaa maalumu kwa lengo la kusimamia masilahi ya wastahiki”.

Kusudio la mali ya Zaka: Ndani yake inakusanya fedha (Sarafu) na zingine katika aina za Zaka kama vile Zaka za mazao ya kilimo matunda wanyama mali ya biashara madini na zisizokuwa hizo.

Kama vile inakuwa wazi kupitia fasiri ya uwekezaji wa Zaka kuwa lengo lake sio tu kufikia faida kubwa katika mali ya Zaka, bali hilo linahusisha na yenye kurejesha faidia kwa wanaostahiki Zaka, kwani uwekezaji wa mali za Zaka hauwi isipokuwa kwa kuangalia masilahi ya wastahiki wake.

*****

Sehemu ya Pili

Hukumu ya Uwekezaji mali za Zaka.

Kuwekeza mali za Zaka ima kupitia kwa mstahiki wake baada ya kuipokea, au kwa mmiliki wake kabla ya kuitoa, au kwa aliyepewa ruhusa na mmiliki wa Zaka kuifikisha kwa wanaostahiki, na katika kila sura katika sura za hukumu zimejitenga katika masuala kama ifuatavyo:   

Suala la Kwanza:

Uwekezaji mali za Zaka kwa upande wa wenye kustahiki.

Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema katika idadi ya aina za watu wanaostahiki zaka:

{Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni wajibu ulio lazimishwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hekima} [AT TAWABAH 60].

Mwenyezi Mungu akataja aina za watu ambao wanafaa kupewa mali za Zaka katika makundi haya manane.

Imamu An-Nasafy anasema katika tafasiri yake: “Zaka imehusishwa na watu wa aina chache, kwa maana yenyewe ni maalumu kwao wala haivuki kwenda kwa wengine zaidi ya wao, kana kwamba imesemwa: Kwa hakika hiyo Zaka ni yao wao tu na wala si kwa wengine” ([12]).

Na Abu Suud naye amesema katika tafasiri yake: “Zaka imehusishwa kwa makundi haya manane na wala haiendi kwa wengine” ([13]).

Masuala ya kuwekeza mali za Zaka kwa upande wa watu wa aina hizi nane kunasimama juu ya kiwango cha nguvu ya umiliki wao wa mali ya Zaka waliyopewa, kwani imepitishwa kwenye kanuni kuwa mwanadamu anaweza kutumia miliki yake vile atakavyo pindipo hakuna madhara ([14]), mwenye kuthibiti kwake umiliki kamili wa mali basi anaweza kuitumia vile anavyotaka katika aina za makubaliano ya kimatumizi, miongoni mwake ni uwekezaji, kwa sababu umiliki kamili unafuatana na matumizi yote, je umiliki wa mali ya Zaka kwa watu wa makundi manane unazingatiwa ni umiliki kamili huru au umiliki dhaifu?

Jibu lake ninasema: Wanachuoni wa Sharia wanatenganisha masuala haya, na kutenganisha kati ya mali iliyotolewa kwa watu wa makundi manne ya mwanzo kutajwa ndani ya Aya – nao ni mafakiri, masikini, wasimamizi wa Zaka, na mwenye kutiwa nguvu moyo wake – na kati ya watu wa makundi mengine manne ya mwisho – nao ni ukomboaji mtumwa, mwenye deni, aliye kwenye njia ya Mwenyezi Mungu na msafiri.

Aina nne za mwanzo Wanachuoni wamekubaliana kuwa umiliki wao wa mali waliyopewa ni umiliki kamili huru, kwani fakiri na wengine katika makundi manne ya mwanzo wanaweza kutumia watakavyo katika aina za matumizi ya mali ya Zaka wanayoimiliki, miongoni mwa matumizi hayo ni pamoja na kuwekeza, ama umiliki wao kamili na huru wa mali ya Zaka ni kuwa haitakiwi kupokonywa baada ya kupewa pindi sifa ya kustahiki kwao ikiondoka.

Imamu Razy anasema katika tafasiri yake: “Fungu la mtumwa hupewa bwana wake kwa kuandikiana, na dalili ya hilo ni kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu amethibitisha Zaka kwa watu wa makundi manne ambayo yemetajwa kwa kutumia herufi ya laam ya umiliki, nayo ni kauli yake: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri}, pindi alipotajwa mtumwa herufi ya Laam ikabadilishwa na kutumika herufi ya Fii, Mola Akasema:  {Na katika kukomboa watumwa} hivyo kwa tofauti hii lazima kutakuwa na faida, na faida hiyo ni kuwa makundi hayo manne yaliyotangulia kutajwa wanapewa fungu lao la Zaka ili waweze kuyatumia watakavyo, lakini kwa upande wa kukomboa watumwa hutolewa fungu lao ili kumalizana na utumwa, na sio kuwezeshwa kutumia mafungu hayo watakavyo, bali huwekwa kwenye mpango wa kukombolewa ili kufanya kazi hiyo, hali kama hiyo kwa watu wenye madeni, hutumika mali ya Zaka katika kulipia madeni yao, na vile vile kwa watu wanaopigania njia ya Mwenyezi Mungu hutolewa fungu la mali ya Zaka kwa ajili ya maandalizi ya vile wanavyohitaji vitani na hata hawa wasafiri, mwisho ni kuwa katika watu wa makundi haya manne ya mwanzo wanapewa mali ya Zaka ili watumie kama wanavyotaka, na watu wa makundi manne ya mwisho hawapewi mali ya Zaka bali wanalipiwa kwenye mahitaji yanayozingatiwa katika sifa ambazo kwa sifa hizo wamestahiki fungu la Zaka” ([15]).

Kana kwamba kinachoangaliwa katika haki ya fakiri, masikini, msimamizi wa Zaka na mwenye kutiwa nguvu moyo wake mambo mawili: Mtu na Sifa, wakati makundi mengine huangaliwa katika haki yao Sifa tu, hivyo Wanachuoni wametofautiana katika hali ya kuondoka sifa ambayo alistahiki mwenye deni au msafiri fungu la Zaka baada ya kutolewa je linaweza kurejeshwa au hapana?

Katika hilo aina ya kundi la kwanza umiliki wao wa mali ya Zaka ni umiliki kamili, na maelezo mengi ya Wanachuoni yameweka wazi katika hilo, kwani Mwanachuoni Ibn Al-Munayyir anasema: “Makundi manne ya mwanzo ni wamiliki wa walichopewa, kwani kutumika kwa herufi ya Laam kunaendana na wao. Ama watu wa makundi manne ya mwisho, hawamiliki wanachopewa wala hawakitumii, isipokuwa kwenye masilahi yanayofungamana nao, mali ambayo hutumika katika kukomboa mtumwa kwa hakika wanapewa muandika uhuru na wauzaji watumwa, wala si fungu lao watumwa kutumia wao wenyewe mpaka lielezewe hilo kwa herufi ya Laam ya umiliki wa kile kinachotolewa kwa ajili yao, kwa kweli ni jambo lisilowezekana matumizi haya na masilahi yanayofungamana nayo, vile vile wenye madeni hutolewa fungu lao kwa ajili ya madeni yao ili kumaliza matatizo yao na wala si fungu lao, ama wapiganaji wa njia ya Mwenyezi Mungu ni wazi katika hilo, ama wasafiri ni kana kwamba wameingizwa katika kundi la wapiganaji wa njia ya Mwenyezi Mungu bali wametajwa peke yao ikiwa ni kuelezewa umaalumu wake” ([16]).  

Sheikh Aliishi katika Masheikh wa madhehebu ya Imamu Maliki anasema katika maelezo yake kuhusu matumizi ya mali ya Zaka kwa wapigania njia ya Mwenyezi Mungu “Ikiwa atakaa” kwa maana: Mgeni akaishi katika nchi ya kigeni baada ya kupewa sehemu ya zaka ili imfikishe nchini kwake “Atanyang’anywa” yaani mgeni mali ya Zaka isipokuwa kwao kama atakuwa ni mtu fakiri, akafananisha katika kupokonya ikiwa atakaa na akasema “Kama mpiganaji” aliyepewa akakaa bila ya kuingia vitani basi atanyang’anywa na kuwa deni kwake kama ametumia hali ya kuwa ni mwenye uwezo, na “Katika” kumnyang’anya “Mwenye deni” kwa maana ya mdaiwa “Anapoajitosheleza” baada ya kuchukuwa na kabla ya kulipa deni lake kwa kuondoka sifa ya kudaiwa na kwa kuchukuwa kwa sura isiyo sahihi, Imamu Lakhmii pake yake ndiye aliyelezea na tamko lake: “Na kwa upande wa mwenye deni atachukuwa kiwango cha kulipa deni lake kisha akajitosheleza kabla ya kulipa deni, lau itasemwa anyang’anywe basi itakuwa na mtazamo, lakini bora zaidi: Ameteua kunyang’anywa mdeni anapojitosheleza” ([17]).

Imekuja katika kitabu cha “Mughny Al-Muhtaaj” katika vitabu vya madhehebu ya Imamu Shaafi: “Imeongezwa kwenye makundi manne ya mwanzo herufi ya Laam ya umiliki, na makundi manne ya mwisho imekuja herufi ya Fii ya kielezi kuonesha umiliki ni kwa makundi manne ya kwanza, na kuzuiliwa umiliki makundi manne ya mwisho, hata ikiwa haijafika zaka katika matumizi yake itarejeshwa tofauti na kundi la mwanzo” ([18]).

Na imekuja katika kitabu cha “Kashaaf Al-Qinaai” ni katika vitabu vya Madhehebu ya Imamu Hambali: “Mwenye kupewa kwa sababu inayokubalika kupewa, nayo ni sababu ya - Ufakiri, umasikini, usimamizi na kuzoeshwa moyo wake -  anaweza kutumia mali ya Zaka vile anavyotaka kama vile anavyotumia mali zake, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ameongeza kwao Zaka kwa kutumia herufi ya Laam ya umiliki, ikiwa atapewa kwa sababu isiyokubalika kumiliki kitachukuliwa alichochukuwa  kwa sababu ya kutothibiti umiliki wake kwa sura zote, ikiwa ametumia kwenye upande ambao unastahiki kuchukuwa hiyo mali, kinyume na hivyo atatakiwa kuirudisha, kama vile anavyochukuwa mwenye kumuandikia mtumwa uhuru, mwenye madeni, mpiganaji na msafiri”  ([19]).

Ama aina nne za mwisho nazo ni – Kumkomboa mtumwa, mwenye deni, aliye katika njia ya Mwenyezi Mungu na msafiri – kumekuwa na tofauti katika kiwango cha umiliki wao wa mali ya Zaka waliyopewa.

Imamu Maliki na Shafi pamoja na Imamu Hambali wanaona kuwa umiliki wao wa mali ya Zaka ni umiliki usio kamili, hivyo huchukuliwa mali ya Zaka kutoka kwa mdaiwa ikiwa atajitosheleza kabla ya kulipa deni lake, au kujivua na deni, au kulipa pasi ya kutumia mali ya Zaka, au kulipiwa na mtu mwingine, ikiwa mpiganaji vita atachukuwa mali ya zaka kisha akakaa bila kutoka kwenda vitani pia itachukuliwa, vile vile huchukuliwa kutoka kwa msafiri ikiwa ataendelea kubaki nchi ya kigeni bila kutoka kwenye nchi hiyo.

Masheikh wa Madhehebu ya Imamu Shaafi wakaondoa ukazi wa mgeni na mpiganaji ili kupata muda wa maandalizi na wakakadiria chini ya siku tatu, na wakasema pia: Lau kitabakia sehemu ya alichopewa msafiri au mpiganaji, msafiri atatakiwa arudishe moja kwa moja, ama mpiganaji atatakiwa arudishe ikiwa amebakiwa na kitu kinachofaa kwa hali ya kawaida bila ya kujifanyia ubahili, na kama hakuna kilichobakia basi hatotakiwa kurudisha.

Watu wa Madhehebu ya Imamu Maliki wakatenganisha kati ya mpiganaji na mgeni katika kuchukuwa kile walichopata katika mali ya Zaka ikiwa mpiganaji hakutoka kwenda vitani au mgeni akaendelea kukaa, basi mgeni ikiwa atakaa bila kutoka kwenye nchi ya kigeni huchukuliwa mali ya Zaka isipokuwa kama atakuwa ni mtu fakiri huko nchini kwake hupewa kwa sifa ya ufakiri, au ikiwa ameshatumia yote basi hatorudisha, ama mpiganaji ikiwa hajatoka kwenda vitani na akatumia ile Zaka aliyochukuwa na akawa ni mtu tajiri basi mali hiyo itakuwa deni kwake halitafutika isipokuwa kwa kulipa.

Sheikh Dardiir amesema katika kitabu cha “Sherhul-Kabiir” alipozungumziwa msafiri: “Ikiwa atakaa” kwa maana akabakia nchi ya kigeni bila kuondoka baada ya kupewa “Atanyang’anywa” isipokuwa kama atakuwa ni mtu fakiri nchini kwake, kama vile “Mpiganaji” akakaa bila ya kwenda vitani pia hunyang’anywa alichopewa na atakuwa na deni kama ameshatumia na akawa ni mtu tajiri, na “Katika” kuchukuwa kwa “Mwenye deni” kwa maana ya mwenye kudaiwa “Anajitosheleza” baada kuchukuwa na kabla ya kulipa deni lake, kutonyang’anywa kwake Sheikh Lakhmy peke yake amesema: Lau itasemwa anyang’anywe basi itakuwa jambo la kuangaliwa, lakini Sheikh Lakhmy ameipa nguvu kauli ya kwanza, ingekuwa bora mtunzi kusema: Kuteua kunyang’anywa mwenye deni anapojitosheleza” ([20]).

Imamu An-Nawawy amesema katika kitabu cha Al-Majmui: “Watu wetu wamesema: Kwa hakika hupewa mwenye deni madam anadeni, ikiwa atalipa au kumalizana nalo basi hapewi kwa sababu ya deni hilo, bali anapewa kiasi kidogo cha mahitaji yake, ikiwa atapewa mali ya Zaka kisha asilipe deni lake bali akamalizana nalo au akalipiwa au akalipa si kwa mali ya Zaka bali ni kwa mali nyingine basi kuna njia mbili: Njia ya kwanza ambayo imepitishwa na mtunzi pamoja na wengine: Ni kuwa atatakiwa kurejesha mali ya Zaka kwa kujitosheleza kulipa deni lake kwa mali nyingine.  Njia ya pili ameielezea Imamu Raafii na wengine: Ni tofauti na ya kwanza katika kuandikiana utumwa, ikiwa amelipiwa deni au amemalizana nalo, na kama atapewa kitu katika mali ya Zaka sehemu ya mali hiyo akalipia deni lake basi kilichobaki kuna njia mbili. Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua zaidi” ([21]).  

Na katika kitabu cha Minhaji na sherehe yake ya Khatibu Sharbiny: “Hupewa mpiganaji na msafiri kwa kauli yao” bila ya ushahidi wala kiapo kwa kauli sahihi, kwa sababu ni jambo la kipindi kijacho “Ikiwa hawakutoka” pamoja na muda wa kujiandaa kwenda vitani na kusafiri “Itatakiwa kurudisha” wote wawili walichochukuwa, kwa sababu sifa ya kustahiki kupewa haijapatikana, jopo la Wanachuoni hawajakadiria muda ambao wanaweza kuchelewa, lakini Imamu Sarkhasy amekadiria siku tatu. Imamu Raafy akasema: Inafananishwa kuwa ni muda wa karibu, kwa maana huchukuliwa kuchelewa kutoka na kufanya maandalizi na mfano wake. Imamu Raafy amesema: Ikiwa atafariki mpiganaji vita akiwa njiani au amejizuia kupigana vita atatakiwa kurudisha kilichobaki, nayo inaonesha kuwa hatorudisha mali yote aliyochukuwa, na hii kama alivyosema Ibn Rafaa ni wazi katika hali ya kufariki kwake lakini si katika kujizuia kwenda vitani.

Ufafanuzi: Maelezo ya mtunzi yanaelezea kuwa mpiganaji vita na msafiri ikiwa wataondoka na wakarejea kisha ikabaki mali ya Zaka basi hawatatakiwa kurudisha, lakini si moja kwa moja bali msafiri atatakiwa kurudisha. Ama mpiganaji vita ikiwa atapigana na akarudi akiwa amebakiwa na sehemu ya mali ya Zaka inayofaa na wala hakujifanyia ubahili basi atatakiwa kurudisha hicho tu kilichobaki, kwa sababu tumebaini kuwa mwenye kupewa amepewa zaidi ya mahitaji yake, lakini ikiwa amejibana au hakujibana na kilichobakia ni kiwango kidogo basi hatorudisha chochote, wala haihusishwi kurudisha kwa hao wawili, isipokuwa ikiwa amepewa mwenye kuandika uhuru wa mtumwa kisha akajitosheleza na kile tulichompa kwa kujitolea bwana wa mtumwa kumuachia huru au kumvua utumwa, kwa kauli sahihi atarudisha alichopewa, kwa sababu makusudio ni kupatikana uhuru kwa mali iliyotolewa” ([22]).

Imamu Bahwaty amesema katika kitabu cha “Kashaf Al-Qanai”: “Na mwenye kuchukuwa mali ya Zaka kwa sababu inayokubalika kuchukuwa – nayo ni ufakiri, umasikini, usimamizi na kuzoeshwa moyo wake – atatumia anavyotaka kama vile anavyotumia mali yake, kwa sababu Mwenyezi Mungu Mtukufu ameongeza kwao Zaka kwa herufi ya Laam ya umiliki, ikiwa atachukuwa kwa sababu isiyokubalika kumiliki hiyo mali hawezi kutumia alichopewa kwa sababu ya kutothibiti umiliki wake kwa namna zote” ([23]).  

Sijaona kwa Masheikh wa Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa – nilivyoangalia kwenye vitabu vyao – andiko kuhusu mwenye deni ikiwa atajitosheleza baada ya kupewa mali ya Zaka, deni lake likaisha kwa kulipa au kutohusika nalo, lakini wamesema kwa upande wa mtumwa: Ikiwa atashindwa kutekeleza makubaliano na makubaliano haya yakavunjwa basi haitarejeshwa mali ya zaka aliyochukuwa, bali inakuwa ni ya bwana wake, kama vile wamesema hivyo kwa msafiri halazimiki kukitoa sadaka kile kilichozidia mkononi mwake baada ya kupewa mali ya Zaka.

Ibn Abedeen anasema: “Amesema pia kwenye kitabu cha Fat’hu: Si halali kwake – kwa maana ya msafiri – kuchukuwa zaidi ya mahitaji yake, na kilichobora kwake kuomba mkopo ikiwa ataweza, lakini si jambo la lazima kwake kukopa kama atashindwa kulipa, wala halazimiki kukitoa sadaka kilichozidia mkononi mwake anapokuwa na uwezo wa mali, kama vile fakiri anapojitosheleza na mtumwa anaposhindwa na wakiwa na mali ya Zaka hawalazimika kutoa sadaka” ([24]).

Inawezekana kuoanisha mwenye deni katika hali hii na mtumwa pamoja na msafiri ambapo hakuna tofauti kati yao, pamoja na deni kuwa ni kitu kinachozingatiwa kuwa lenyewe linapelekea kustahiki fungu la zaka, basi je anaweza kuendeleza mali ya Zaka aliyochukuwa kwa ajili ya kulipa deni lake?

Kwa kauli za watu wa Madhehebu ya Imamu Maliki na Imamu Shaafi pamoja na Imamu Hambali ni haifai, isipokuwa watu wa Madhehebu ya Imamu Shaafi wamesema inafaa kwa mtumwa na mwenye deni kufanyia biashara mali ya Zaka waliyochukuwa ikiwa kutafuta ongezeko na kutekeleza, lakini hii ikiwa atapewa kidogo zaidi ya thamani ya mkataba wa uhuru au kiwango cha deni, basi inafaa kwake kuwekeza ili ifikie kiwango kinachostahiki, na Imamu Nawawiy anasema: “Hili halina tofauti” ([25]).

*****

  Suala la Pili:

Kuwekeza mali za Zaka kwa upande wa mmiliki wake kabla ya kutoa.

Mwenye kumiliki mali ya Zaka anaweza kukuza mali yake baada ya kuwajibika mali hiyo kutolewa Zaka na kabla ya kuitoa, hili linaleta matatizo nayo ni kuwekeza mali za Zaka kutapelekea mali kuchelewa kufika kwa mstahiki wake, hivyo utoaji Zaka inapowajibika inapaswa kutolewa haraka au kwa kuchelewesha?

Jibu la maswali haya tunasema: Lengo la kuzungumzia je Zaka ni wajibu wa kutelekezwa haraka au kucheleweshwa ni kuwa uwekezaji mali za Zaka unapingana na utoaji zaka haraka na kuendana na ucheleweshaji, mazungumzo ya ulipaji Zaka haraka na kuchelewesha ni utangulizi wa maelezo ya kwa namna gani mwenye mali iliyofikia kiwango cha kutolewa Zaka inafaa kuwekeza.

Wanachuoni wametofautiana zaka kuwa ni wajibu wa kutekelezwa haraka au kwa kucheleweshwa, kwani Jamhuri ya Wanachuoni wanasema kuwa zaka ni wajibu wa kutekelezwa haraka, ikiwa mtu anamiliki kiwango cha kutoa Zaka na kutimia masharti ya Zaka ni lazima atoe na atapata dhambi kwa kuichelewesha, haya ni makubaliano kati ya Jamhuri ya Wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa – katika Fatwa yao – pamoja na Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Maliki Imamu Shaafi na Imamu Hambali ([26]).  

Imamu Shaafi na Imamu Hambali wakaondoa hali ya uharaka ikiwa mtu atachelewa kwa udhuru, kama vile kusubiri kuitoa kwa mtu wa karibu au mtu mwema au jirani, Imamu Hambali akazidisha ikiwa amehofia kuitoa haraka kwa sababu ya madhara kwake mwenyewe au kwenye mali yake, lakini Imamu Shaafi ameweka sharti katika kuchelewa kutoleta madhara makubwa kwa waliopo wanaostahiki kupewa, na kama si hivyo basi haifai kuchelewesha na itatolewa kwa wale waliopo, na Imamu Shaafi akaongeza kuwa kuchelewesha bila udhuru baada ya kuwezekana kutekeleza inapaswa kuwepo kitu cha dhamana ikiwa itaharikibika.

Jamhuri ya Wanachuoni wakachukuwa dalili ya kutolewa zaka haraka kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na toeni Zaka} [AL BAQARAH 43].

Sehemu ya dalili: Ni kuwa Aya imeamrisha kutoa, na amri ya moja kwa moja inatekelezwa haraka.

Kama vile wamechukuwa dalii ya Hadithi ya Bibi Aisha R.A amesema: Mtume S.A.W amesema: “Haichanganywi mali ya Zaka isipokuwa itaisha” ([27]). Al-Humaidy amesema: “Inaweza kuwa imewajibishwa kwako katika mali yako Zaka kisha usitoe haramu huangamiza halali, na Mwenyezi Mungu ndiye Anayejua zaidi hali”.

Pia wakasema: Mahitaji ya mafakiri ni kufanikiwa, hivyo wajibu unapaswa kutekelezwa haraka, kama vile Zaka ibada inayojirudia kila mwaka, wala haifai kucheleweshwa mpaka wakati mwingine wa lazima wa mfano wake kama vile Swala na funga ([28]).

Na kwa Maimamu wa madhehebu ya Abu Hanifa wanasema kuwa: Zaka inapaswa kutolewa kwa kucheleweshwa na wala si kwa haraka. Al-Kasaany anasema katika kitabu cha Badaai Swanaai: “Maana ya kuchelewesha kwao wao, ni kuwa inawajibika si ndani ya wakati maalumu, wakati wowote ule akitoa Zaka anakuwa ametekeleza wajibu, na huainishwa wakati huo wa wajibu, ikiwa hajatoa Zaka mpaka mwisho wa umri wake wajibu unambana kwa kubakia wakati kiasi cha kuweza kutoa Zaka na akadhania kuwa ikiwa hatatoa ndani ya huo wakati atakufa na kupitwa, katika hali hiyo ikiwa hatatoa Zaka mpaka anakufa atapata dhambi ([29]).

Imamu Al-Kasany katika tofauti na masuala haya amerejesha tofauti kwenye masuala ya msingi, nayo yanapelekea amri ya wakati, nayo ni masuala maarufu katika misingi ya Fiqhi lakini kuna kauli tofauti, iliyopitishwa – kama alivyosahihisha Imamu Razy na Imamu Al-Aadamiy na Ibn Haajib na wengine – kuwa amri iliyoepukana na dalili haifungamani na uharaka, bali inaonesha kutakiwa kutekelezwa jambo ([30]).

Kauli yake Mola Mtukufu: {Na toeni Zaka} haioneshi uharaka wa kutoa, bali inaonesha utoaji wa Zaka umepukana na wakati.

Na Hadithi ya Bibi Aisha R.A haioneshi uharaka, kauli ya Al-Humaidy si yenye kuelezea tafasiri ya Hadithi, Ibn Hajar Al-Asqalany baada ya kutaja maelezo ya Al-Humaidy anasema: “Tafasiri hii kusudio ni jambo la kheri, hivyo ndivyo ninavyoelewa maelezo ya Al-Humaidy, na inachukuliwa kuwa kwa mwingine miongoni mwa waliojuu yake, na kusudio linachukuliwa kuwa mtu anachukuwa Zaka na yeye tajiri na kuongeza kwenye mali yake isipokuwa itapotea, na haya yameelezwa na Imamu Ahmad na kwa maelezo hayo nimeyapitisha kuyapokea kwenye mlango huu ([31]) ([32]).

Pamoja na hayo rai ya Jamhuri ya Wanachuoni hapa ndio yenye nguvu, lakini kwa dalili nyingine, nayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na toeni haki yake siku ya kuvunwa kwake} [AL AN'AAM 141]. Nayo ni amri inayofungamana na wakati, na amri inayofungamana na wakati inapelekea kujirudia na uharaka ([33]).

Kutokana na hayo haifai kwa mmiliki wa mali ya Zaka kuchelewesha – Ikiwa amewajibika – pasi ya udhuru, na wala sio kuwekeza, lakini ikiwa atachelewesha kwa udhuru miongoni mwa nyudhuru zilizotangulia na kuongezeka, kama vile kuzaliwa kwa mbuzi, au kupanda bei ya sarafu, hivyo kwa mwenye kuwa na ongezeko hili, ikiwa atachelewesha kwa udhuru je anaweza kuwekeza?

Jibu la swali hii linatokana na kanuni: “Mali kwa dhamana” kanuni hii inakubaliana na kauli ya Jamhuri ya Wanachuoni kuwa kutoa Zaka ni wajibu wa kutekelezwa haraka, kwa sababu mwenye kusema kutolewa kwa kucheleweshwa kwani Zaka kabla ya kutolewa haijaainishwa mali yake, kwani mali yote kabla ya kuitoa ni miliki yake hivyo anaweza kuiwekeza, ama mwenye kusema haraka na ilihali mmiliki wa Zaka amechelewa kuitoa kwa udhuru, Imamu Shaafi ameelezea kuwa ikiwa itaharibika mali ya mtoa Zaka inadhaminiwa, ikiwa hivyo anaweza kuiwekeza kwa kufuata kanuni ya mali kwa dhamana, na maana yake ni kuwa: “Kutoa kitu kunakuwa kwa yule aliyeharibu hicho kitu inakuwa kwenye dhamana yake, kama vile kilichouzwa kinapokabidhiwa kwa mnunuzi kisha akakirudisha kwa kuwa na kasoro, inakuwa mali yake kwa sababu kama kitapotea mikononi mwake kinakuwa kwenye dhamana yake na ataibeba” ([34]).

****

Suala la Tatu:

Uwekezaji mali za Zaka kwa msimamizi au anayekaimu nafasi yake.

Wanachuoni wamekubaliana juu ya uhalali wa msimamizi mkuu au anayekaimu nafasi yake kukusanya Zaka, na kumuondolea jukumu mtoaji, Imamu au anayekaimu nafasi yake anasimamia ugawaji kwa wanaostahiki, lakini kwa sababu za kupanuka eneo la nchi za Kiislamu na kuwepo kwa taasisi nyingi ambazo zinafanya kazi ya kukusanya Zaka, na uwingi wa fedha zinazokusanywa kwenye taasisi hizo, baadhi ya hizo taasisi zimejielekeza kupeleka mali za Zaka katika miradi ya kiuwekezaji inayosimamia – kwa mtazamo wa taasisi hizi – kulinda mali za Zaka kama mitaji ya miradi hii, na kukidhi kwa njia nzuri haja za mafakiri masikini na wenye kuhitaji zaka, ambapo humbadilisha huyu muhitaji kutoka mpokeaji wa mali ya Zaka na kuwa mzalishaji, kuongezea pia faida za kiuchumi ambazo zinarejea kutoka kwenye hiyo miradi hasa miradi ikiwa ya kiuzalishaji.

Masuala haya katika kadhia za Zaka ndani yake wametofautiana Wanachuoni wa leo kati ya kutoruhusiwa na kuruhusiwa, wapo waliosema inafaa kama vile: Jopo la Kimataifa la Wanachuoni wa Sharia ya Kiislamu na baadhi ya Taasisi za Kisharia na Taasisi za Zaka, kama vile Taasisi ya Kisharia ya Baitul-Zakati nchini Kuwait, na Baitul-Tam’wiily ya Kuwait, pia Taasisi ya Uhasibu na Marejeo Taasisi ya fedha ya Kiislamu ([35]). Wakati ambapo waliona mfumo huu haufai ni pamoja na: Jopo la Sharia la Makka, na Jopo la Sharia ya Kiislamu nchini India.

Wanachuoni waliopinga na wale walioruhusu wametoa dalili zinazokubali kujadiliwa, miongoni mwa dalili za wanaopinga ni kama zifuatazo:

Kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:  {Wa kupewa sadaka ni mafakiri} Aya.

Sehemu ya dalili: Kuwekeza mali za Zaka kutapelekea kuwapa watu wasiokuwa wa makundi haya, nalo ni jambo linalokwenda kinyume na maelekezo ya Aya ([36]).

Inajadiliwa dalili hii kusema kuwa, uwekezaji mali ya Zaka hakuna utoaji Zaka na kuwapa wasiostahiki, bali asili ya mali na mapato yake ni kwa ajili ya wanaostahiki, mali ya uwekezaji inayotolewa ni jitihada ya namna ya kugawa na wala si jitihada kwa anayepewa, kisha kunufaika kunakozuiliwa ni kunufaika bila badala yeyote kama vile kuchukua faida ya mradi mtu asiyestahiki bila ya badala yeyote, ama kunufaika kwa malipo hakuna ubaya, bali ni katika mambo yanayolazimu kuendeshea miradi, mfano wa hilo ni baadhi ya matajiri kufanya kazi katika miradi hii, mshahara anaochukuwa kwa kazi anayoifanya ndani ya mradi unakuwa ni sehemu ya fungu la wanaosimamia uendeshaji wa mali za Zaka, na masuala haya ni katika mitazamo mipya ya ibada ya Zaka. Kauli ya mwisho ni kuwa uwekezaji wa mali za Zaka huenda kutapelekea kuitoa na kuwapa wasiostahiki na kupaswa kupokea.

Kuwekeza mali ya Zaka kunapelekea kuchelewa kuwafikia wanaostahiki, na kuwanyima uwezo wa kukidhi mahitaji yao ya asili mpaka pale mradi utakapopata faida, nalo ni jambo tofauti na uharaka uliowekwa kama sharti ya Zaka ([37]). Na inazungumzwa kuwa uharaka hapa ni kwa mmiliki wa Zaka kuitoa, wala si sharti kwa kiongozi au kaimu wake, kwani anaweza kuchelewa kugawa, na dalili ya hilo: Hadithi iliyopokelewa na Anas Ibn Maliki amesema: “Nilikwenda kwa Mtume S.A.W nikiwa na Abdillah Ibn Abi Twalha ili kumbariki kwa kumrambisha tende, nikampatia mkononi mwake chuma cha kuwekea alama ngamia wa zaka” ([38]).

Ama kauli ya kuwekeza kunapelekea kuwazuia wanaostahiki kukidhi mahitaji yao ya asili mpaka wasubiri faida, hili linaweza kumalizwa kwa kutoanzisha miradi kama hii ila baada ya kumaliza mahitaji muhimu ya wastahiki, kama vile chakula na mavazi, ipo wazi kabisa kuwa lau fakiri atapewa hiyari kutoshelezwa hivi sasa na mali ya Zaka kwa kupewa yote mara moja, na kati ya kukidhi baadhi ya mahitaji yake asili na mali iliyobaki iwekezwe jambo linalopelekea kujitosheleza kipindi chote cha mwaka, kwa hakika atachagua hiyari ya pili.

Uwekezaji mali za Zaka kunapelekea hasara, hivyo hupotea mali za wastahiki ([39]). Katika hili hakuna kinachojificha miongoni mwa udhaifu, kwani Sharia imehimiza kuwekeza mali za yatima pamoja na kuwepo hatari ya kupatikana hasara, kama ilivyokuja katika Hadithi: “Ifanyieni biashara mali za mayatima wala msiile zaka” kisha haijifichi kuwa kuangalia ubora wa miradi na idara zake ni katika vigezo vya mafanikio na kuepuka hasara.

Kuwekeza mali za zaka kwa upande wa kiongozi au kaimu wake kunapelekea kutomiliki wastahiki wa Zaka, nalo ni jambo linalokinzana na umiliki uliowekewa sharti katika kutekeleza Zaka ([40]).

Hili linazungumziwa kuwa uwekezaji wa mali za Zaka haimaanishi kutomiliki wastahiki wa Zaka, kwa sababu imechukuliwa kuwa vifaa vya miradi kuanzia mashine vifaa na visivyokuwa hivyo si vya wastahiki, hili si sahihi, kwani mtaji wa mradi na faida yake ni miliki ya wastahiki, lengo lililopo ni serikali kukaimu nafasi yao katika uendeshaji mradi, nayo inafanana sana na makampuni yenye hisa ambapo wenye hisa ndio wamiliki na wala si wakurugenzi.

Pia katika dalili hii inaweza kupingwa kuwa umiliki si katika masharti ya utoaji zaka, kwani baadhi ya Wanachuoni wamepitisha kutoa Zaka bila mmiliki katika baadhi ya hali ([41]).

Dalili za waliopitisha ni zifuatazo:

Hadithi ya Anas R.A kuwa watu kutoka Arinah walienda Madina na Mtume S.A.W akawaruhusu walete ngamia wa Zaka wapate kunywa maziwa yao.

Upande wa dalili ni kuwa: Mtume S.A.W hakugawa Zaka kwa wastahiki kwa haraka, bali alichelewesha na kuwekeza kinachozalishwa miongoni mwa kuzaana kukamua maziwa na kupewa wastahiki ([42]).

Hadithi ya Anas Ibn Maliki kuwa mtu mmoja katika watu wa Ansar aliendewa na Mtume S.A.W akamuuliza: “Je nyumbani kwako kuna kitu chochote?” akasema: Ndio, vazi hili sehemu tunavaa na sehemu nyingine tunatandika, na chombo tunanywea maji. Mtume S.A.W akasema: “Niletee hivyo vitu viwili” akavileta. Mtume S.A.W akavichukuwa kwa mkono wake na akasema: “Nani atanunua vitu hivi?” mtu mmoja akasema: Mimi nitanunua kwa Dirham moja. Mtume S.A.W akasema tena: “Nani atazidisha kwa Dirham mbili?” akauliza mara mbili au tatu, yule mtu akasema: Mimi nitavichukuwa kwa Dirham mbili, akapewa na Mtume S.A.W akachukuwa Dirham mbili akampa yule Ansar na akamuambia: “Dirham moja nunua chakula ulishe familia yako, na Dirham nyingine kanunue shoka kisha unilietee”, yule mtu akanununua shoka na kuileta, Mtume S.A.W akalifunga mpini kwa mkono wake kisha akamuambia: “Nenda kakate kuni na uuze nisikuone isipokuwa baada ya siku kumi na tano”, yule mtu akaenda kukata kuni na kuuza kisha akaja kwa Mtume S.A.W akiwa na Dirham kumi baadhi yake akanunua nguo na baadhi ya zingine akanunua chakula. Mtume S.A.W akasema: “Hii ni bora kwako kuliko kuja kuomba kwani kuombaomba ni dowa katika uso wako siku ya kiyama, hakika kuomba hakufai isipokuwa kwa watu watatu: Mwenye umasikini uliokithiri, mwenye madeni ya kutisha, mwenye damu ya maumivu”.

Sehemu ya dalili: Ni kuwa ikiwa imefaa masikini kuwekeza mali yake inayoshughulikia mahitaji yake asili, inafaa kwa kiongozi kuwekeza mali za Zaka kabla ya kuzigawa kwa wastahiki ([43]).

Lakini hili linaongelewa kuwa hakuna kinachoonesha kiongozi kuwekeza mali za zaka, bali kinachoonesha ni masikini kufaa kuwekeza mali yake hata kama anahitaji, ingefaa kufanya dalili ya kiongozi kuwekeza mali za Zaka kama Mtume S.A.W angechukuwa mali ya Zaka na kuiendeleza, na hakuna linaloonesha hilo.

Upanuzi wa matumizi katika njia ya Mwenyezi Mungu, baadhi ya Wanachuoni wamepitisha kuwa kutumia mali ya Zaka katika njia ya Mwenyezi Mungu inakusanya mambo yote mazuri ya umma ([44]), ikiwa inafaa kutumia mali ya Zaka katika masilahi ya umma au mambo ya kheri, basi inafaa kuitumia kujengea miradi ya kiuwekezaji ambayo itarudisha faida kwa wastahiki.

Kulinganisha uwekezaji wa mali za Zaka na wasia wa kuendeleza mali za mayatima, kwani yote mawili ni katika aina za kuendeleza kuna hofu na wasi wasi wa kuharibika au kutumika, ikiwa inafaa kuendeleza mali za mayatima nazo ni miliki zao za kweli, basi vile vile inafaa kiongozi kuwekeza mali za Zaka nazo ni miliki za wastahiki mali na faida ([45]), na uwingi wa mali za zaka kwenye Taasisi zilizo na jukumu la kukusanya kunatoa fursa kwa hizo Taasisi kufanya uwekezaji huu.

Linganisha uwekezaji wa mali za Zaka kwa upande wa msimamizi wa mambo katika kuwekeza mali za waqfu, zote hizo mbili ni mali zinahusu haki za wengine na kukusudiwa ukaribu kwa Mwenyezi Mungu, kama vile inafaa kukuza mali za waqfu na kuendeleza pia inafaa kuwekeza mali za Zaka ([46]).

Lakini hii inazungumziwa kuwa kuna tofauti kati ya mali ya Waqfu na mali ya zaka, mstahiki wa waqfu hamiliki mali ya Waqfu, bali anastahiki faida yake, tofauti na mali ya Zaka kwani mtaji wa mradi – kama upo – na faida yake ni miliki ya mstahiki.

Ulinganisho wa kuchelewesha mali ya Zaka kwa kuiwekeza na kuitoa haraka kwa maslahi ya wastahiki ili kuhudumia mahitaji yao ([47]). Lakini hujadiliwa hili kuwa kuharakisha – pamoja na kutofautiana – isipokuwa maandiko yanasema inafaa, tofauti na kuchelewasha hakuna andiko linalopitisha.

Kuongeza mtaji wa wastahiki wa Zaka kwa mali za zaka ni maslahi ya kweli kwa msimamizi wa mambo ya jamii kwa uongozi wake, afanye kazi ya kuhakiki ongezeko hili, kwa maamuzi anayoona ni njia ya kufikia ([48]).

Kauli yenye nguvu:

Baada ya kuelezea dalili za wanaopinga na wanaopitisha, na upingaji ambao umetolewa na dalili kwa pande zote mbili, kile kinachoonekana, lakini elimu ya uhakika wake ni ya Mwenyezi Mungu, ni kuwa kauli ya kufaa kuwekeza mali za Zaka kwa kiongozi au kaimu wake kuna mitazamo inayokabiliana nayo, hasa dalili za waliopitisha hazijasalimika na kupingwa, kama vile kulinganisha kiongozi /Imamu kuwekeza mali za Zaka na kiongozi wa jamii kuwekeza mali ya mayatima, kama vile matumizi ya kiongozi/Imamu aliyopewa kwa masilahi, hakuna shaka kuwa kuendeleza mali kwa namna hii ndani yake kuna masilahi yasiyofichika, linaongezwa katika hilo kuwa kufaa sio moja kwa moja, bali kuna udhibiti lazima ufikiwe, na haya ndio yaliyopitishwa na kongamano la tatu la kadhia za kisasa za Zaka, baada ya kujadili tafiti zilizotangulia kwenye maudhui hii imemalizikia kuwa, yafaa kuwekeza mali za Zaka kwa vigezo vifuatavyo:

Kusiwepo pande za kupewa zinazopelekea ugawaji wa haraka wa mali za Zaka.

Uwekezaji wa mali za Zaka ufanyike – kama uwekezaji mwingine – kwa kufuata njia halali.

Kuchukuliwa hatua sahihi za kubakia mali inayowekezwa katika asili ya hukumu ya Zaka na vile vile faida ya mali hiyo.

Kufanya haraka kutoa kidogo kidogo mali inayowekezwa pale itakapohitajika kwa mahitaji ya wastahiki wa Zaka kupewa.

Kufanya juhudi ili uwekezaji ambao utaingiziwa mali za Zaka kuwa ni wenye kuwezekana salama na kuweza kutoa kidogo kidogo pale inapohitajika.

Kuchukuwa maamuzi ya kuwekeza mali za Zaka wale waliopewa mamlaka na kiongozi kukusanya zaka na kuzigawa kwa kuangalia msingi wa Kisharia, na usimamizi wa uwekezaji wapewe watu wenye uwezo uzoefu na uaminifu([49]).  

  *****

Ambatisho la Maazimio ya Majopo ya Fiqhi na Vyombo vya Kisharia

Waliopitisha:

Jopo la Kimataifa la Fiqhi ya Kiislamu litokanalo na Jumuiya ya Ushirikiano wa nchi za Kiislamu:

Azimio nambari: 15 (3/3) kuhusu: Zaka kutumika katika miradi yenye faida bila kumilikiwa na mtu anayestahiki Zaka.

Tamko la Azimio:

“Baraza la Jopo la Fiqhi ya Kiislamu katika mkutano wake wa tatu uliofanyika Oman mji mkuu wa Jodan kuanzia mwezi 8 – 13 mfungo tano 1407H, sawa na tarehe 11- 16 October 1986, baada ya kuangalia utafiti uliowasilishwa katika maudhui ya kutumia mali ya Zaka kwenye miradi yenye faida bila ya umiliki wa mtu anayestahiki, na baada ya kusikiliza mitazamo na rai za wajumbe pamoja na wataalamu, yaliazimiwa yafuatayo:

Kwa mujibu wa msingi inafaa kutumia mali za zaka kwenye miradi ya uwekezaji inayomilikiwa na watu wenye kustahiki Zaka, au mradi kuwa chini ya usimamizi wa Taasisi ya Kisharia yenye kuhusika na ukusanyaji wa Zaka na ugawaji wake, baada ya kushuhurikia mahitaji muhimu ya haraka ya wastahiki, na kuwepo dhamana ya kutosha ili kuepuka hasara.

Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kujua Zaidi

*****

Fatwa namba (94) ya mwaka 2011 ofisi ya Mufti wa Misri.

Tamko la Fatwa:

 Je inafaa mimi pamoja na kundi la wafanya biashara kuanzisha mradi wa kiuwekezaji kwa mali za Zaka faida yake itapelekwa kwa watu mafakiri na masikini, na hilo ili sisi itupe nafasi ya kuwa na chanzo cha mapato cha kudumu ili kuwapa wao?

Jibu: Asili ya mali za Zaka ambazo mtoaji anapotoa au kufika mikononi mwa kiongozi au anayekaimu nafasi yake katika taasisi za Zaka ni kufanya haraka kuzigawa kwa wastahiki wala haifai kuchelewesha, kwani Wanachuoni wa Fiqhi wamesema, kiongozi au mtu anayepelekwa kukusanya Zaka kwa hakika ni muwakilishi wa wastahiki, kama ilivyokuja kwenye kitabu cha Mughny Al-Muhtaj (1/413 chapa ya Al-Halaby), lakini ikiwa dharura au haja au masilahi ya wastahiki vimepelekea kuchelewesha kuzigawa basi hakuna ubaya kuchelewesha, na inaondolewa pia katika asili iliyopita kufaa kuchelewesha kwa ajili ya uwekezaji, ikiwa dharura au mahitaji yanapelekea hivyo, kama vile kulinda rasilimali asili za wastahiki, kuimarisha nafasi za kazi kwa wasio na ajira miongoni mwa wastahiki, basi inafaa kuwekeza katika miradi ya uzalishaji, lakini linafaa hilo kwa masharti matatu:

Sharti la Kwanza: Uwekezaji wa mali za Zaka ulete masilahi ya kweli kwa wastahiki: Kama kulinda chanzo cha kudumu kinacholeta maisha bora kwao.

Sharti la Pili: Mwenye mali ya Zaka iliyowajibika kwake kutoa kutokana na umiliki, na mradi utamilikiwa na mafakiri, kwa kufanya kazi kwa mfano kama shirika au kampuni ya wanahisa na hisa zake kumilikiwa na mafakiri, na umiliki hautokuwa wa mwenye mali ambaye ametoa Zaka, bali lazima mali za Zaka zitoke kwenye umiliki wake na kwenye jukumu lake, kama si hivyo basi mali hiyo inakuwa ni waqfu na sio zaka, na sharti la kumiliki mafakiri linaonekana katika uwazi wa Aya Tukufu:

{Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni wajibu ulio lazimishwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hekima} [AT TAWBAH 60].

Herufi ya Laam ina maanisha umiliki, Mwanachuoni Al-Khatib amesema ndani ya kitabu cha “Mughny Al-Muhtaj” (4/173 chapa ya Dar Al-Kutubi Al-Ilmiya): “Katika makundi manne ya mwanzo imeongezwa herufi ya Laam ya umiliki, na makundi manne ya mwisho imekuja herufi ya Fii ya kielezi ili kuonesha umiliki upo kwa makundi manne ya kwanza na si makundi manne ya mwisho, hata Zaka isipofika katika makundi yake itarudishwa, tofauti na kundi la kwanza”.

Ugawaji wa Zaka umehusishwa na makundi haya tu, Imamu An-Nasafy amesema katika tafasiri yake (1/688): “Zaka imehusishwa kwa makundi machache, kwa maana yenyewe imehusishwa kwao tu bila ya kuvuka kwenda kwa wengine, kana kwamba imesemwa kwa hakika Zaka ni kwa ajili yao tu na si kwa wengine”.

Na Imamu Sarkhasy amesema katika kitabucha Al-Mabsuutw (2/202 chapa ya): “Asili ni kuwa wajibu ni kitendo cha kutoa sehemu ya mali, na wala hakuna utoaji isipokuwa kwa umiliki, kila kijiji kikikosa umiliki hakipaswi kutoa Zaka”.

Katika kitabu cha Durru Al-Mukhtar cha Ibn Aabideen 2/344 chapa ya Darul-Fikri: “Imewekwa sharti la kuwa cha kutolewa miliki na wala si uhalali, wala haitoshi kulisha isipokuwa kwa njia ya umiliki, lau atalisha alichonacho kwa nia ya Zaka haitoshi, vile vile kila asichomiliki”. 

Sharti la Tatu: Kuchukuliwa hatua zote ambazo zinapelekea mafanikio ya hiyo miradi baada ya kumiliki kikamilifu wastahiki wa kupewa Zaka, wala faida yake haitatolewa isipokuwa kwao tu.

Wanachuoni wa Fiqhi wa madhehebu ya Imamu Shaafi pamoja na Imamu Hambali – nayo ndiyo Fatwa iliyopitishwa kama ilivyoelezwa – wamesema inafaa kuwekeza mali za Zaka kwa upande wa wastahiki baada ya kukabidhiwa, kwa sababu Zaka pindi inapofikishwa mikononi mwao inakuwa miliki yao kamili, hivyo inafaa kutumia kama wamiliki wanavyotumia miliki zao, wanaweza kuanzisha miradi ya kiuwekezaji, kununua vifaa vya kazi na vitu vyengine.

Imamu wa Misikiti Miwili amesema katika kitabu cha “Nihaayatil-Matwlab” 11/533 chapa ya Daarul-Minhaaj: “Waislamu wamekubaliana kuwa Zaka ni zenye kufanyiwa kazi katika mali za matajiri na walio katika maana kama yao, lengo kuu kugawa sehemu ya mali za matajiri na kuwapa Waislamu wenye kuhitaji…. Na makusudio ya Sharia kuondoa mahitaji kwa mali za Zaka”.

Kisha Imamu wa Misikiti Miwili akasema juu ya kufaa mwenye kustahiki Zaka kuanzisha mradi na kuusimamia kwa mtaji unaotosha, na akasema katika kitabu cha “Nihaayatil-Matwlab” 11/545: “Kwa watu masikini wanapaswa kuchukuwa kiwango kinachotosha pato lake kutoa, wala haukadiriwi muda wa mwaka, kwani ambaye anamiliki Dinar ishirini akazifanyia biashara, na pato lake halitoshi kutoa kwa sasa huyo ni masikini, ikiwa alichonacho mikononi mwake kinatosha kwa mwaka, basi kinachozingatiwa ni kutoa mali inayompatia kipato kinatosha kukitoa, ikiwa hawezi kugawa basi kilichokaribu ni kummilikisha kinachomtosha katika umri wake, ikiwa ana umri wa miaka kumi na mitano na katika mwaka anahitaji kiasi cha kumi, kutapelekea kumkusanyia mali nyingi zisizoendana na kanuni za kawaida za kutosheleza, kilichokaribu na Fiqhi: Ni kuwa ikiwa anauwezo mzuri wa kufanya biashara tutammilikisha mali inayomtosha kutumia, na kama si mzuri kwenye biashara tutamuwekea orodha ya kufanya biashara”.

Na Sheikh Abu Is’haka Shiirazy amesema katika kitabu cha “Al-Muhadhabu” 1/324 chapa ya Daarul-Kutubi Al-Ilmiya: “Mtu fakiri ni yule ambaye hana kinachomtosheleza anapewa kile kitakachomuondelea mahitaji yake ikiwa ni pamoja na vifaa vya kufanyia kazi kama ana nguvu au bidhaa ataifanyia biashara hata kama atahitaji mali nyingi za bidhaa ambazo zinamfaa yeye na kufanya vizuri biashara basi lazima apewe”.

Na Mwanachuoni Al-Bahuty Al-Hambaly amesema katika kitabu cha Kashaf Al-Qinai 2/282 chapa ya Daarul-Kutubi Al-ilmiya: “Kanuni ya madhehebu kama alivyotaja Al-Majdi kuwa mwenye kuchukuwa Zaka kwa sababu zinazokubalika kuchukuwa, nazo ni ufakiri umasikini usimamizi na uzoeshwaji moyo, atatumia atakavyo kama anavyotumia mali zake”, kwa sababu Mwenyezi Mungu ameongeza kwao kwenye neno la Zaka herufi ya Laam ya umiliki, na ikiwa amechukwa kwa sababu zisizokubalika kwa maana ya kutothibiti sababu za umiliki, ikiwa atatumia kwa pande ambazo zinastahiki kuchukuwa, na kama si hivyo basi atatakiwa kurejesha, kama anavyochukuwa muandikaji uhuru wa mtumwa, mwenye deni, mpiganaji na msafiri, kwa sababu Mwenyezi Mungu ameongeza kwao neno la Zaka herufi ya Fii, nayo ni kielezi, kwa sababu watu wa makundi manne ya mwanzo wanachukuwa kwa maana ya kuchukuwa, nayo ni kuwatosheleza mafakiri masikini wazoeshwa mioyo yao na malipo kwa wasimamizi wa zaka, na wasio kuwa hao wanachukuwa kwa maana haipo kwenye kuchukuwa zaka basi hutengenishwa”.

Kwa maelezo hayo na kwa mujibu wa swali: Ni kuwa inafaa kuanzisha miradi ya kiuwekezaji kwa mali za Zaka kwa masharti yaliyoelezwa.

*****

Kongamano la tatu la Kadhia za Zaka:

Tamko la Azimio:

Washiriki katika kongamano la tafiti iliyowasilishwa katika maudhui ya uwekezaji mali za Zaka walijadili na kufikia maazimio yafuatayo:

Kongamano linasisitiza maazimio ya Jopo la Fiqhi ya Kiislamu nambari 3/3/7/86 kuhusu kufanyia kazi mali za Zaka kwenye miradi yenye faida, ni jambo linalofaa kwa baadhi ya udhibiti ulioelezwa na azimio.

Baada ya mjadala wa tafiti iliyowasilishwa kwenye kongamano katika maudhui hii kuhusu msingi na udhibiti walifikia yafuatayo:

Yafaa kuwekeza mali za Zaka kwa udhibiti ufuatao:

Kusiwepo pande za kupewa kinachopelekea ugawaji haraka wa mali za Zaka.

Uwekezaji wa mali za Zaka ufanyike – kama uwekezaji mwingine – kwa kufuata njia halali.

Kuchukuliwa hatua sahihi za kubakia mali inayowekezwa katika asili ya hukumu ya Zaka na vile vile faida ya mali hiyo.

Kufanya haraka kutoa kidogo kidogo mali inayowekezwa pale itakapohitajika kwa mahitaji ya wastahiki wa Zaka.

Kufanya juhudi ili uwekezaji ambao utaingiziwa mali za Zaka kuwa ni wenye kuwezekana salama na kuweza kutoa kidogo kidogo pale inapohitajika.

Kuchukuwa maamuzi ya kuwekeza mali za Zaka wale waliopewa mamlaka na kiongozi kukusanya Zaka na kuzigawa kwa kuangalia msingi wa Kisharia, na usimamizi wa uwekezaji wapewe watu wenye uwezo uzoefu na uaminifu”.

*****

4-Chombo cha Uhasibu na marejeo cha Taasisi ya fedha ya Kiislamu.

Vipimo maalumu vya Kisharia vya Zaka nambari: 35.

 Tamko la Kipimo:

10- Hukumu za utoaji Zaka:

10/2- Asili ya utoaji zaka baada tu ya kuwajibika kuitoa, na inafaa kuichelewesha kuitoa kwa muda usiozidi mwaka.

10/4- Asili ya kutumia Zaka katika makundi yake, na wakati wa kuhitajika inafaa kufanyiwa kazi mali za Zaka katika miradi ya kiuwekezaji inayoishia kumilikiwa na watu wanaostahiki Zaka, au kuwa chini ya taasisi ya Kisharia yenye jukumu la kukusanya mali za Zaka na kuzigawa, hilo baada ya kukamilisha mahitaji muhimu ya haraka ya wastahiki na kuwepo dhamana za kutosha ili kuepuka hasara.

*****

Wanaopinga:

Jopo la Fiqhi ya Kiislamu la Jumuiya ya Waislamu Ulimwenguni:

Azimio nambari: 88/6/15: Kuhusu uwekezaji mali za Zaka.

Tamko la Azimio:

“Shukrani zote anastaki Mwenyezi Mungu peke yake, sala na salamu ziwe kwa Nabii wa mwisho, naye ni Mtume wetu Muhammad S.A.W

Baada ya Utangulizi:

Baraza la Jopo la Kifiqhi ya Kiislamu la Jumuiya ya Waislamu Ulimwenguni katika kikao chake cha kumi na tano kilichofanyika Makka ambacho kilianza siku ya Jumamosi mwezi 11 mfungo kumi 1419H, sawa na tarehe 31/10/1998, liliangalia maudhui ya uwekezaji mali za Zaka, na baada ya kujadili na kuzingatia hukumu za utoaji Zaka na pande zake za kupewa Baraza limeazimia yafuatayo:

Zaka inapaswa kutolewa haraka, na hilo ni kwa kumiliki wastahiki kupewa waliopo wakati wa kuwajibika kutolewa, wale ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesimamia kuainisha kwa Aya ya Kitabu chake, Akasema Mola Mtukufu:

{Wa kupewa Zaka ni mafakiri na masikini} [AT TAWBAH 60]

Kwa Aya hii, haifai kuwekeza mali za Zaka kwa masilahi ya yeyote katika wastahiki – kama vile mafakiri – kwa kuwepo tahadhari mbali mbali za Kisharia, miongoni mwazo: Ukiukaji wajibu wa kutolewa haraka, na kupitwa umiliki wake kwa wastahiki wakati wa kuwajibika kutolewa, na madhara kwao.

Rehma na amani zimuendee Mtume wetu Muhammad pamoja na watu wa nyumbani kwake na Maswahaba zake.

Shukrani zote anastahiki Mola wa viumbe vyote.

*****

Jopo la Fiqhi ya Kiislamu nchini India:

Azimio nambari 53/2/13 kuhusu uwekezaji mali za Zaka.

Tamko la Azimio:

“Washiriki katika kongamano baada ya kupitia maudhui ya tafiti iliyowasilishwa, na baada ya kusikiliza kwao mjadala na mitazamo ya Wanachuoni na wataalamu, na kwa kuangalia maazimio ya baadhi ya Majopo ya Kifiqhi waliazimia yafuatayo:

Kwanza: Waislamu kuchelewa kwenye mambo ya Uchumi ni jambo lisilo hitaji maelezo, na kutokana na hilo walinganiaji wa Kikristo na wa Kikadiani pamoja na makundi yaliyodhidi ya Uislamu wanatumia umasikini wa Waislamu na ujinga wao, na wanafanya juhudi kubwa kuwapotosha Waislamu katika dini yao na imani yao kwa kushirikiana nao kiuchumi, lazima kupambana na hali hii hatari na kufanya juhudi kubwa za kuondoa umasikini wao na kuboresha hali zao kiuchumi pamoja na kuwaokoa kutoka katika makucha ya maadui, miongoni mwa majukumu ya Waislamu sehemu zote ni pamoja na kuwasaidia Waislamu mafakiri kwa mali za Zaka, ikiwa mali za Zaka hazitatosha kwa mahitaji yao basi ni jukumu lao kushirikiana nao kwa mali zingine kutoka mifuko mingine na katika mali za kujitolea.

Pili: Mali za Zaka ambazo hutolewa kwa kuwapa mafakiri na masikini zinawapatia haki zote za umiliki, na kutokana na hilo fakiri ikiwa atawekeza au kuziingiza kwenye biashara au kununua hisa ili kunufaika nazo ndani ya kipindi kijacho hilo linafaa kwake.

Tatu: Ili kufikia lengo la kumfanya fakiri na masikini wajitosheleze wao wenyewe katika uchumi ikiwa itanunuliwa mashine au chombo cha uzalishaji kwa mali za Zaka kwa kuangalia ujuzi wao, au kufunguliwa maduka na wakapewa kwa kumilikishwa hilo nalo linafaa, na hilo linakamilisha utoaji Zaka kwa watu wake.

Nne: Lau zitajengwa nyumba au kufunguliwa maduka kwa mali za Zaka na kukabidhiwa watu masikini na mafakiri ili waishi au wafanye biashara humo, na wakipewa bila kumilikishwa hilo halifai.

Tano: Kisharia haifai kuweka mali za Zaka katika miradi ya kiuwekezaji ikiwa pamoja na kuanzisha viwanda na makampuni ili kugawa faida zake kati ya watu wanaostahiki kupewa mali za Zaka, ni sawa sawa limefanywa hilo na watoa Zaka wenyewe au pande za Kisharia zinazohusika na kazi za ukusanyaji wa Zaka na kugawa, kwa sababu mali za Zaka kwa sura hii hazifiki kwa wastahiki wake, na inahofiwa kiwanda kupata hasara na kupotea fedha nyingi za zaka, kuongezea pia kujizuia kukidhi mahitaji muhimu na ya haraka ya wastahiki pamoja na kugandisha mali za Zaka.

Sita: Miongoni mwa majukumu ya watoa Zaka na pande za Kisharia zinazohusika na kazi za ukusanyaji Zaka na kuzigawa kuzipeleka kwanza kwa wahitaji na wastahiki katika maeneo yao, na kuwapa ili kukidhi mahitaji yao.

Matokea ya Tafiti

Mwisho wa tafiti nimefikia yafutayo:

Kusudio la uwekezaji mali za Zaka: “Ni kukuza na kuendeleza kupitia vyombo maalumu kwa lengo la kusimamia masilahi ya wastahiki”.

Hukumu ya uwekezaji mali za Zaka hutofautiana kwa kutofautiana muwekezaji, na hilo ni kama ifuatavyo.

Kwanza: Ikiwa uwekezaji unafanywa na wastahiki Zaka baada ya kupewa, basi kuna hali mbili:

Ikiwa mstahiki ni mtu fakiri au masikini au mfanya kazi katika taasisi ya kukusanya Zaka au ni katika wenye kuzoezwa nyoyo zao, basi Wanachuoni wamekubaliana kuwa umiliki wao wa mali waliyopewa ni umiliki kamili na huru, wanaweza kutumia miliki zao za Zaka vile watakavyo, ikiwa ni pamoja na uwekezaji.

 Ikiwa mstahiki si katika makundi haya ya kupewa Zaka Wanachuoni wametenganisha na kila kundi limefafanuliwa hapo nyuma.

Pili: Ikiwa uwekezaji ni kwa upande wa mmiliki wa mali ya Zaka kabla ya kuitoa kwa ajili ya Zaka, basi haifai kwake kuwekeza.

Tatu: Ikiwa uwekezaji ni kwa upande wa Kiongozi au anayekaimu nafasi yake, kauli yenye nguvu ni inafaa kuwekeza kwa masharti yaliyotajwa hapo nyuma.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

*****

Orodha ya Marejeo Muhimu

“Sahihi Bukhary” Al-Jaami Al-Musnad Sahihil-Mukhtasar katika mambo ya Mtume S.A.W na Sunna zaka pamoja na masiku yake, cha Imamu Muhammd Ibn Ismail Al-Bukhary. Uhakiki umefanywa na Muhammad Zuheir Nasir, chapa ya Dar Twauku Najat “Uchapishaji na Sultania kuongezea uwekaji namba umefanywa na Muhammad Fuad Abdulbaky, juzuu ya kwanza, 1422H.

“Sahihi Muslim” Al-Musnadu Sahihil-Mukhtasar, upokezi sahihi unaotakana na usahihi mpaka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W cha Imamu Muslimu Ibn Al-Hajaj An-Nisaabury, uhakiki: Muhammad Fuad Abdulbaky chapa ya Dar Ihyaai Turathil-Araby.

Tafiti na kazi za kongamano la tatu la kadhi za kisasa za zaka, zimesambazwa kwenye tovuti ya mfuko wa zaka nchini Lebanoni: www.zakat.org.Ib

Uwekezaji mali za zaka Dr. Muhammad Othman Shubeir – ni katika jumla ya tafiti za Kifiqhi katika kadhia za kisasa za zaka.

Kitabu cha Asnal-Matwalib sherehe ya Rawdhul-Twalib, cha Sheikh Zakaria Al-Ansar, chapa ya Dar Al-Kitabu Al-Islamy.

Kitabu cha Al-Intisaf minal-Kashaf, cha Mwanachuoni Ibn Muniir As-Sakandary, uhakiki: Adil Abdulmawjud na Ally Muawadh, chapa ya Maktaba Al-Abikan 1418H, 1998.

Al-Insaf fii Maarifatul-Rajih minal-Khilaf, cha Alaa Diin Al-Mardawy, chapa ya Dar Ihyaai Turathil-Araby.

Al-Bahrul-Muhitw fii Usuul Al-Fiqhi, cha Imamu Badrudeen Zarkashy, uhakiki: Sheikh Abdulkadir Al-Any, marejeo: Dr. Omar Al-Ashqar, chapa ya Dar Al-Kutuby nchini Misri.

Badaii Swanaaii, cha Kasany, chapa ya Darul-Kutubil-Imiyah.

Basair Dhawi Tamyiiz fii Latwaif Al-Kitabil-Aziz, cha Majdideen Al-Fairuuz Aabady, uhakiki: Muhammad Najjar, chapa ya Baraza kuu la mambo ya Kiislamu – Tume ya kuhuhisha urithi wa Kiislamu – Kairo.

Al-Binayah Sherhu Al-Hidaya. Cha Badrudeen Al-Ainy, chapa ya Darul-Kutubil-Imiyah, chapa ya kwanza  1420H 2000.

Tabyeen Al-Hakaik sherhu Kanzu Dakaik, cha Zailay, chapa ya Darul-Kitabil-Islaamy.

Tuhfatul-Muhtaj sherhul-Minhaj – kikiwa na ufafanuzi wa Ibn Kassim Al-Ibady na Abdulhamid Sharwany Al-Daghastani – cha Ibn Hajar Al-Haitamiy, chapa ya Daru –Ihayai Turathil-Al-Araby.

Tafsiir Nasaqy “Madaaraku Tanziil wa Hakaiku Taawiili”, uhakiki: Yusuf Badyawy chapa ya Darul-Kalami Tayyib, chapa ya kwana 1419H 1998.

Haashiyatu Dusuuqy Alaa Sherhi Sayyidyy Ahmad Al-Dardiry Alaa Mukhtasar Khalil, chapa ya Daru Ihyaai Al-Kutubil-Arabia.

As-Sunanul-Kubraa, cha Imamu Al-Hafidhi Abibakri Al-Baihaqy, uhakiki: Muhammad Abdulkadir Atwa, chapa ya Darul-Kutubil-Alamiyah.

Fat’hul-Baary Sherhu Sahihi Al-Bukhary, cha Haafidh Ibn Hajar Al-Asqalaany, uhakiki: Muhammad Fuad Abdulbaky na Muhibbu Deen Al-Khatib, chapa ya Dar Al-Maarifah Beirut.

Fat’hul-Qadiir, cha Kamal Ibn Al-Hammam, chapa ya Darul-Fikri.

Kaamus Al-Iqtisaady, cha Dr. Muhammad Bashir, chapa ya Taasisi ya Al-Arabiyah ya tafiti na usambazaji, nchini Beirut, chapa ya kwanza 1985.

Lisaanul-Arab, cha Ibn Mandhwur, chapa ya Darul-Swadir, chapa ya tatu 1414H.

Jarida la Ahkaam Al-Adiliya, utunzi: Tume inayoundwa na idadi ya Wanachuoni na Wanafiqhi katika zama za utawala wa Othaman, uhakiki: Najib Hawawiiny, chapa ya Nuur Muhammad, Karakhanah Tajaarati Kutubi, Aaram Baagh, Karatch.

Jarida la Jopo la Kimataifa la Sharia ya Kiislamu.

Sherhul-Muhadhibu, cha Imamu Muhyideen An-Nawawy, chapa ya Darul-Fikri.

Musnadi Al-Humaidy, cha Abibakri Al-Humaidy Al-Makky, uhakiki: Hassan Asad, chapa ya Darul-Saqaa, Damascus, chapa ya kwanza 1996.

Matumizi ya zaka na kumiliki katika wigo wa Qurani na Sunna, cha Khalid Abdulrazik Al-Aany, chapa ya Daru Usama, nchini Jodan, chapa ya kwanza 1999.

Matumizi katika Njia ya Mwenyezi Mungu, cha Dr. Mustafa Abdulkareem, kimechapishwa kwenye Jarida la Ofisi ya Mufti wa Misri, toleo la pili, mfungo mosi 1430H. October 2009.

Al-Matwalibul-Aaliyah Bizawaaidi Al-Masaaniid Thamaniyah, cha Al-Hafidh Ibn Hajar Al-Asqalaany, kwa ushirikiano na: Dr. Saad Al-Shashry, chapa ya Darul-Aswimah, Darul-Ghaithi nchini Saudi Arabia, chapa ya kwanza 1419H.

Al-Muujamu Al-Wasiitwi, ya Jopo la Wataalam wa lugha ya Kiarabu, Jijini Kairo, chapa ya Darul-Daawah.

Muujam Miqyaas Lughat, cha Abil-Hussein Ibn Faris Al-Qadhawiiny Raazy, uhakiki: Abdulsalaam Harun, chapa ya Darul-Fikri, 1399H – 1979.

Maalamatu Zaid cha kanuni za Kifiqhi.

Mughny Al-Muhtaaj Ilaa Maarifati Al-Faadhiy Al-Minhaaj, cha Khatibu As-Sharbiiny, chapa ya Darul-Kutubil-Ilimiyah.

Al-Mughny Sherhu Mukhtasar Al-Kharqy, cha Ibn Qudamah Al-Maqdisy, chapa ya Daru Ihyaai Turathil-Araby.

Mafaatiihul-Ghaibi, cha Imamu Fakhrudeen Razy, chapa ya Daru Ihyaai Turathii Al-Araby, chapa ya tatu, 1420H.

Al-Mufradat fii Gharib Al-Quran, cha Raaghib Al-Asfahany, uhakiki: Safwan Daudy, chapa ya Darul-Qalam, chapa ya kwanza, 1412H.

Al-Manshuur fii Qawaaid, cha Imamu Badrideen Zarkashy, uhakiki: Dr. Taisiir Faaiq, chapa ya pili: 1405H, chapa ya Wizara ya Waqfu nchini Kuweit.

Manhil-Jaliil, Sherhu Mukhtasar Khaliil, cha Sheikh Muhammad Aliish, chapa ya Darul-Fikri.

Mausuuatu Al-Mustwalahaat Al-Iqtisaadiyah, cha Dr. Hussein Omar, chapa ya Darul-Shuruuq, Jiddah, chapa ya tatu 1399H.

Nihaayatul-Suul, Sherhu Minhaajil-Wusuul, cha Imamu Jamal Deen Al-Istiwaa, chapa ya Darul-Kutubil-ilmiyah, chapa ya kwanza 1420H – 1999.

Nihaayatul-Matwalib fii Diraayatil-Madh’abi, cha Imamul-Haramaini Al-Juwainy, uhakiki: Dr. Abduladhiim Diib, chapa ya Darul-Minhaaj.

 

[1] Kitabu cha Lisaanu Al-Arab 4/106, na Kamusi ya viwango vya lugha 1/388.

[2] Kitabu cha Nihaayatul-Matwlabi 8/10.

[3] Kitabu cha Tabyiin Al-Hakaik 6/220.

[4] Al-Binaya sherehe ya Al-Hidaya 11/501.

[5] Kitabu cha Asnaa Matwalib 2/393.

[6] Kitabu cha Badaai Swanaaii 2/5.

[7] Kamusi ya kiuchumi ya Dr. Bashir Aliyyah ukurasa wa 33.

[8][8] Kamusi elezo ya kiuchumi ya kundi la wanachumi ukurasa wa 38.

[9] Kamusi ya misamiati ya kiuchumi ya Dr. Hussein Omar ukurasa wa 33.

[10] Rejea fasiri hizi katika utafiti wa Dr. Muhammad Saleh Hamdy kwa anuani: “Maana ya uwekezaji katika uchum”,

[11] Kamusi ya Al-Wasiit ukurasa 100

[12] Tafasiri ya Imamu An-Nasafy 1/688.

[13] 4/76.

[14] Al-Mushiir 3/236 na jarida la hukumu za kiuadilifu 1/230- mada 1192.

[15] Kitabu cha Mafatih Al-Ghaibu 16/86.

[16] Kitabu cha Al-Insaaf 3/60.

[17] Kitabu cha Manhi Al-Jalil 2/92.

[18] 4/173.

[19] 2/282.

[20] 1/498.

[21] 6/209.

[22] 4/184.

[23] 2/282.

[24] 2/343.

[25] Kitabu cha Al-Majmuui 6/204.

[26] Rejea kitabu cha Fat’hul-Qadiir 2/153 na kitabu cha Imamu Dusuqy cha sherhul-Kabiir 1/500 na kuendelea. Pia kitabu cha Mughny Al-Muhtaaj 2/136, na kitabu cha Al-Insaaf 3/186.

[27] Imepokewa na Baihaqy katika kitabu cha Al-Kubra 4/268, na Al-Hamidy katika musnadi yake 1/275.

[28] Rejea kitabu cha Al-Mughny 2/290.

[29] Rejea: 2/3.

[30] Rejea: Kitabu cha Al-Bahrul-Muhitw 3/311, na kitabu cha Nihayatul-Suul ukurasa 135.

[31] Inakusudiwa mlango wa “Kukataza kuoimba kwa asiyehitaji” nayo yanakubaliana na yaliyoelezwa katika tafasiri ya kuchanganya zaka ya mali.

[32] Kitabu cha Matwalibul-Aaliya 5/589.

[33] Rejea: Al-Bahrul-Muhiitw 3/317.

[34] Rejea: Utafiti wa Dr. Muhammad Ruuky kuhusu kanuni mali kwa dhaman 14/380.

[35] Maelezo ya pande hizi yatakuja mwishoni mwa utafiti.

[36] Rejea: Utafiti wa Dr. Hassan Al-Amin katika jarida la Jopo la Kimataifa la Wanasheria wa Kiislamu, toleo la tatu sehemu ya kwanza.

[37] Marejeo yaliyopita, utafiti: Uwekezaji mali za zaka wa Dr. Muhammad Othman Shubeir 2/518 ni katika jumla ya tafiti za Kifiqhi katika kadhia za kisasa za zaka.

[38] Imekubaliwa na Wanachuoni wa Hadithi, imepokelewa na Imamu Bukhary katika kitabu cha mambo ya zaka, mlano wa kiongozi kumuweka alama ngamia wa zaka kwa mkono wake. Na imepokewa na Imamu Muslimu kitabu cha: Vazi na pambo, mlango: Inafaa wanyama kuwaweka alama.

[39] Rejea utafiti wa Adam Abdillah katika jarida la jopo la Kimataifa la Wanasharia ya Kiislamu, tolea la tatu sehemu ya kwanza.

[40] Rejea utafiti wa Muhammad Othman katika jarida la jopo la Kimataifa la Wanasharia ya Kiislamu, tolea la tatu sehemu ya kwanza.

[41] Rejea: Kitabu cha uwekezaji mali za zaka cha Dr. Muhammad Othman Shubair 2/522.

[42] Marejeo yaliyopita 2/519.

[43] Marejeo yaliyopita 2/521.

[44] Rejea utafiti wa: Matumizi katika njia ya Mwenyezi Mungu” wa Dr. Mustwafa Abdulkareem, uliochapishwa kwenye jarida la ofisi ya Mufti wa Misri, toleo la pili mfungo mosi 1430H sawa na mwezi October 2009.

[45] Rejea utafiri wa Dr. Mustafa Zarka katika jarida la Jopo la Kimataifa la Sharia za Kiislamu, chapa ya tatu, sehemu ya kwanza.

[46] Rejea: Utafiti wa uwekezaji wa mali za zaka wa Dr. Muhammad Othman Shubeir 2/522.

[47] Rejea utafiti wa: Matumizi ya zaka na umiliki wake, wa Khalid Al-Aany ukurasa wa 544.

[48] Rejea utafiti wa: Matumizi ya zaka na kumiliki ukurasa wa 344.

[49] Rejea: Tafiti na kazi za kongamano la tatu la kadhia za kisasa za zaka, zimechapishwa kwenye tovuti ya mfuko wa zaka nchini Lebanon: www.zakat.org.Ib

Share this:

Related Fatwas