Fungu la Zaka
Question
Ni lipi fungu la Zaka ya bidhaa za ya biashara?
Answer
Zaka ya bidhaa za biashara huhisabiwa kwa kutoa jumla ya mali inayotakiwa kuwepo kwenye mzunguko katika jumla ya mtaji.
Sharti la mali ya mtaji kufikia kiwango (Nacho ni sawa na gr 85 ya dhahabu ya aina ya 21).
Inawezekana kufupisha hilo kwa kutumia mchanganuo ufuatayo:
Kiwango cha zaka ya biashara = (Thamani ya bidhaa iliyopo kwa bei iliyopo sokoni + fedha zilizopo mkononi mwa mfanya biashara + deni linalotakiwa kulipwa – madeni ya mtoa Zaka kwa mwingine) x (2.5%) (Asilimia ya Zaka iliyofikisha mwaka wa Kiislamu) au (2.577) (Kwa mujibu wa mwaka wa kawaida).
Thamani inakuwa kwa kila mfanya biashara kwa hesabu yake, ni sawa sawa akiwa ni mfanya biashara wa jumla au rejareja, na bei ya kati na kati kwa mwenye kuuza jumla pamoja na rejareja.
Ofisi ya Mufti wa Misri inatoa nasaha kufahamu mtaji unaofanya kazi katika hali zote kutokana na umuhimu wa kufanyiwa marejeo na mapitio na Wahasibu.