Kuswali kwa haraka

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuswali kwa haraka

Question

Ni kipi kikomo cha haraka kinachoathiri usahihi wa Swala? 

Answer

Kuswali kwa haraka kwa kiasi kinachoathiri usihihi wa Swala ni kile kiasi cha kuhama kutoka nguzo moja hadi nyingine pasipo na kutulia, jambo ambalo Wanafiqhi wanaliita utulivu, ambako ni: kutulia kwa viungo vyote vya mwili kwa muda katika nguzo zote za Swala, kama vile; anayeswali kutulia katika rukuu na kusujudu kwake kwa muda wa kutosha kusema (Subhan Rabbi Al-Adhim) katika rukuu, au (Subhan Rabbi Al-A’ala) wakati wa kusujudu, kwa mara moja kwa uchache, basi Muislamu akitimiza nguzo akatulia na kutuliza viungo vya mwili wake kwa kadri ya utulivu, basi Swala yake ni sahihi, wala haraka hapa haiathiri usihihi wa Swala au kuibatilisha.

Share this:

Related Fatwas