Kulipa Deni kwa Mali za Zaka

Egypt's Dar Al-Ifta

Kulipa Deni kwa Mali za Zaka

Question

Muulizaji anasema kwamba mtoto wa mama yake mdogo amekopa pesa ili imwezeshe kupata nyumba kutokana na kuanguka nyumba yake, na hali yake haimwezeshi kulipa pesa hiyo, na anauliza, je! Kunajuzu kulipa deni lake kwa kukopa mali ya Zaka?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Zaka inatolewa kwa watu wa aina nane waliotajwa katika Qurani Tukufu: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima}[Al-Tawba, 60], na kati ya watu wanaopewa Zaka ni wenye badeni ambao hawawezi kulipa, Imamu Abu Hanifa amesema katika aina hii: Mwenye deni ni yule ambaye hana pesa ya kulipa deni lake, na kumpa pesa ili alipe deni lake ni bora kuliko kuwapa mafukara na masikini, wafuasi wa Madhehebu ya Malik wanasema: Mwenye madeni, ni yule ambae anadaiwa na hana uwezo wa kulipa deni lake, hivyo deni lake linalipwa kwa mali ya Zka baada ya kifo chake, wafuasi wa Madhehebu ya Hanbali wanasema: Wenye madeni wamegawanyika sehemu mbili:

Sehemu ya kwanza aliyekopa kwa ajili ya kuwasaidia watu.

Wa pili aliyekopa kwa ajili ya kujisaidia mwenyewe katika jambo la halali au la harama, na akatubu, atapewa cha kulipa deni lake, na Wanazuoni wa Madhehebu ya shafi wamesema: Mwenye madeni ni yule ambaye ameshindwa kulipa deni, na katika rai za Wanazuoni wa Fiqhi wanaona kwamba kunajuzu kumpa Zaka mwenye madeni ili alipe madeni yake.

Na katika yaliyosemwa linapatikana jibu la muulizaji.

Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi.

Share this:

Related Fatwas