Kuwapa wazazi waliokufa malipo ya Sadaka
Question
Ni ipi hukumu ya kuwapa wazazi malipo ya sadaka baada ya kufa kwao?
Answer
Mwenyezi Mungu Mtukufu amefanya iwe ni wajibu kuwaheshimu wazazi wa mtu na kuwafanyia wema katika sehemu nyingi. Miongoni mwao ni kauli yake Mola Mlezi: “Na Mola wako Mlezi ameamrisha kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu, na wazazi wawili muwatendee wema. Mmoja wao akifikia uzee, naye yuko kwako, au wote wawili, basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee. Na sema nao kwa msemo wa hishima. Na uwainamishie bawa la unyenyekevu kwa kuwaonea huruma. Na useme: Mola wangu Mlezi! Warehemu kama walivyo nilea utotoni” [Al-Isra: 23-24].
Sehemu ya kuwaheshimu wazazi wa mtu ni kutoa sadaka na kuwapa ujira wa sadaka, hasa ikiwa ni sadaka inayoendelea, inawafikia. Imepokelewa kutoka kwa Imaam Al-Bukhari katika “Sahih” yake kutoka kwa Abdullah bin Abbas, (R.A): “Mtu mmoja alimwambia Mtume (S.A.W): Mama yangu amefariki. Je, itamfaa nikitoa sadaka kwa niaba yake? Akasema: “Ndio mimi ninalo bustani, na ninashuhudia kwenu kwamba nimetoa bustani hilo kwa ajili yake.”