Kuuza dhahabu na fedha kwa malipo y...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuuza dhahabu na fedha kwa malipo ya awamu.

Question

Ipi hukumu za kuuza dhahabu na madini ya fedha kwa malipo ya awamu kwa kuongeza thamani katika bei ya asili?

Answer

Kununua dhahabu au madini ya fedha zilizochapwa na kuuza kwa malipo ya awamu kwa thamani yote au kwa muda wa baadaye na ongezeko la thamani kwa sababu ya kulipa kwa muda wa baadaye unaofahamika na uliokubaliwa wakati wa makubaliano, hakuna zuio lolote Kisharia, kwa sababu inafaa kuuza kwa bei ya sasa hivi au kwa bei ya baadaye kwa muda unaofahamika, na ongezeko linalofahamika katika bei kutokana na malipo kufanyika baada ya muda ni jambo linalofaa Kisharia, na kwa vile dhahabu na fedha zimekuwa ni bidhaa kama bidhaa zingine, na kukosekana sababu ya kifedha ambayo inawajibisha sharti la kufanana na sharti la kufika muda na kukabidhiana mezani.

Share this:

Related Fatwas