Fiqhi na Sharia
Question
Ni nini tofauti kati ya Fiqhi na Sharia?
Answer
Kwa kweli tofauti kati ya Fiqhi na Sheria ni kwamba sharia ni kanuni na misingi ya jumla inayotokana na Qur`ani Tukufu na Sunna za Mtume (S.A.W.) ikiwemo hukumu za kiutendaji, kiimani, kitabia, kimiamala na kuzipanga kwa watu wenyewe kwa wenyewe na kwa watu mbele ya Mola wao, hali ya kuwa Fiqhi hujikita zaidi hukumu za kisharia tu, nayo ni kazi ya Maimamu wenye jitihada na uwezo wa kuchukua hukumu kutokana na vyanzo vya sharia kwa karne kadhaa, hata hivyo, Fiqhi hukusanya hukumu zilizo thabiti na zinazobadilika badilika kulingana na mabadiliko ya hali ya mambo katika jamii lengwa.
Kwa hiyo, sharia ni hukumu za kiujumla zilizo thabiti, lakini Fiqhi ni hukumu maalumu zinazobadilika na kujengewa jitihada na tafakari, pia, sharia ni wajibu wa Muislamu kuamini na kutekeleza, kwa hiyo Muislamu anapaswa kuwajibika sharia; hukumu, imani, tabia na mwenendo, hali ya kuwa Muislamu huruhusiwa kuchagua Madhehebu miongoni mwa mojawapo ya Madhehebu za Maimamu wa Fiqhi.
Aidha, sharia huwa inafaa wakati na mahali popote, lakini Fiqhi ni jitihada ambazo huenda kufaa wakati au mahali fulani bila ya kufaa pengine kutokana na maana ya istilahi yenyewe, mbali na hayo kutofautisha Fiqhi na jitihada kwa upande wa dhana ya kila upande, ingawa Fiqhi ni sehemu ya sharia kwani Fiqhi ni kuelewa sharia na matokeo ya jitihada pamoja na kuzitekeleza.