Walii na Uwalii

Egypt's Dar Al-Ifta

Walii na Uwalii

Question

Walii ni nani? Na namna gani Waislamu walifanyia kazi masuala ya uwalii na mwenye kudai uwalii?

Answer

Walii ni mja mwema ambaye Mwenyezi Mungu anampa kutokana na ibada zake utiifu waka na kujiweka kwake karibu na Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu humpa mja uwalii kwa huruma zake upole wake na ulinzi wake, nafasi zao zimethibiti ndani ya Qur`ani na Hadithi, kwani Mwenyezi Mungu Anasema:

{Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na hofu wala hawatahuzunika} Yunus: 62.

Na Mtume S.A.W. anasema:

“Hakika katika waja wa Mwenyezi Mungu kuna watu si Manabii wala Mashahidi bali Manabii na Mashahidi siku ya Kiyama watatamani kuwa kama hao kutokana na nafasi zao walizopewa na Mwenyezi Mungu Mtukufu. Maswahaba wakauliza: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu tufahamishe ni nani hao, Mtume S.A.W. akasema: Hao ni watu wamependana kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hawana undugu kati yao, wala hawana mali wanazopeana, basi ninaapa kwa Mwenyezi Mungu nyuso zao zina nuru, na wao wana nuru, hawana hofu pindi watu watakapokuwa na hofu, wala hawahuzuniki pindi watu watakapohuzunika” akasoma hii Aya:

{Jueni kuwa vipenzi vya Mwenyezi Mungu hawatakuwa na hofu wala hawatahuzunika}. Hadithi imepokewa na Abu Daud.

Mtume S.A.W. alipata kuulizwa:

Ni wakina nani hao Mawalii wa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Ni wale wanapoonekana humtaja Mwenyezi Mungu”. Hadithi imepokewa na An-Nisai.

Waislamu walifanyia kazi masuala ya Uwalii kwa imani kuthibitisha na kukiri uwepo wa Mawalii kutokana na kujiweka kwao karibu na Mwenyezi Mungu, na kwa wenye kudai uwalii walipuuzwa na kufutwa utajo wao na athari zao.

Share this:

Related Fatwas