Kusikiliza nyimbo

Egypt's Dar Al-Ifta

Kusikiliza nyimbo

Question

Ipi hukumu ya kusikiliza nyimbo na vipi vigezo vya Kisharia katika hilo?

Answer

Kuimba kama kuimba katika Sharia ya Kiislamu si haramu, kwani zimepokewa Hadithi nyingi ambazo zimebainisha Mtume S.A.W. kukubali kwake nyimbo na mashairi pamoja na uwimbaji katika mambo yasiyokuwa ya maasi, kama vile ilivyokuja katika Hadithi ya Bibi Aisha amesema:

“Mtume S.A.W. aliingia ndani mimi nikiwa na wajakazi wawili wakiimba, Mtume S.A.W. alilala kitandani na kugeuza uso wake, akaingia Abubakri R.A akashangaa na akasema: Kuna zumari za kishatani nyumbani kwa Mtume S.A.W. ndipo Mtume akamuangalia Abubakri na akasema: Waache” Hadithi imekubalika na wapokezi wote. Mtume S.A.W. hakukataza kuimba kwa wajakazi wawili jambo linaloonesha ni halali kuimba kwa maneno kujipa raha nafsi zao siku ya mnasaba na ulikuwa ni mnasaba wa Eid, kuimba maneno mazuri ni uzuri na kuimba maneno maovu ni uovu, Kisharia hakuna kizuizi cha kusikiliza wimbo kwa vigezo maalumu, kama vile kuwa hauleti hisia za matamanio na kulingania katika hayo, na katowasahaulisha na wajibu wa wakati wa ibada, vile vile hali kama hiyo kwenye nyimbo ambazo zinaenda na mziki, kwani mziki ni sauti, iliyo nzuri ni nzuri na iliyombaya ni mbaya, ikiwa vitachungwa vigezo hivyo hivyo Kisharia inakuwa halali na wala hakuna ubaya kusikiliza. 

Share this:

Related Fatwas