Kuondoa Maovu

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuondoa Maovu

Question

Je, Makundi ya kigaidi yanatekeleza kuamrisha mema na kukataza maovu?

Answer

Kuondoa maovu ni wajibu katika sheria ya kiislamu, lakini kwa masharti maalumu na kuondolewa na wenye mamlaka na watawala, namna na njia za kuondoa maovu ni nyingi kwa ajili ya kufikia mema, pia, huenda kutokea madhara katika juhudi za kuondoa maovu kama vile; kutumia silaha n.k. kwa hiyo, sheria ya kiislamu imeainisha viwango vya kuondoa maovu, pia, Wanachuoni wamefafanua vidhibiti na masharti hayo kwa urefu wakizingatia matini husika.

Ikitokea haja ya kutumia silaha, basi ni jukumu la mtawala kuondoa maovu endapo hakuna njia nyingine inayofaa kutimiza jambo hilo, isije kupelekea maovu na madhara makubwa zaidi kuliko maovu yanayotakiwa kuondolewa, miongoni mwa dalili ya hayo kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua} [Al-Ana'am: 108], ambapo kuepukana na madhara ni muhimu zaidi kuliko kutafuta maslahi.

Kuondoa na kukataza maovu huwa kwa mkono kwa mtawala, na kwa watu wengine huwa kwa kutumia mawaidha, kwa hiyo Muislamu anapaswa kujitahidi kuondoa maovu iwezekanavyo, lakini awe mpole, ambapo upole huchangia kukubaliwa na kuelewana na wengine, pia, Muislamu anaruhusiwa kuomba msaada wa wengine kuondoa maovu akiwa hahofii fitina au fujo kwa kutumia silaha au kuzuka vita au mzozo usio na udhibiti, akishindwa kudhibiti zoezi la kuondoa maovu, basi amwakilishe mtawala au mamlaka husika, akishindwa kufanya lolote, basi ayakatae kwa moyo wake.

Share this:

Related Fatwas